Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama ngombe wa kisasa wakati alipotembelea shamba la ng’ombe wa
maziwa la MILKCOM TANZANIA LIMITED lililopo Kigamboni jijini Dar es
salaam. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni Januari 4, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa eneo la Kisarawe Two
wilayani Kigamboni wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipozungumza nao baada ya kukagua wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni
ya mafuta ya OILCOM kijijini hapo. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara ya
wilaya hiyo Januari 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama kitanda wakati alipotembelea wodi ya wazazi iliyojengwa na
kampuni ya mafuta ya OILCOM katika ENEO la Kisarawe Two wilayani
Kigamboni, Januari 4, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya
Kigamboni, Hashim Mgandilwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni