Jumatano, 22 Februari 2017

SERIKALI YA ANDAA MPANGO WA AJIRA KWA VIJANA .

Tokeo la picha la antony mavunde

Naibu waziri wakazi vijina ajira nawatu wenye ulemavu nchini Antony Mavunde

 

Timothy Marko .
KATIKA kuhakikisha tatizo la ajira kwavijana linatafutiwa ufumbuzi serikali imesema inatarajia kuanzisha mpango maalum wa mafunzo kwa vijana unaoendana sambamba naujuzi wamaswala mbalimbali ikiwemo sekta yaviwanda ilikuwawezesha vijana hao kujiajiri nakuajiriwa katika taasisi mbalimbali nchini .

Akizunguza katikaufunguzi wampango endelevu wa kuwapatia vijana ujuzi jijini Dar es salaam Naibu waziri wakazi vijina ajira nawatu wenye ulemavu nchini Antony Mavunde amesema mpango huo wamiaka mitano unaotarajiwa kuanza hivi karibuni utawawezesha vijana kupata mafunzo mbalimbali ilikuwawesha vijana hao kuingia katika soko la ajira bila kikwazo chakukosa ujuzi .

''Serikali tayari imeshawapeleka vijana mbalimbali katika viwanda vyanguo ilikuweza kupata ujuzi katika sekta ya viwanda napia tunayo programu maalum kwavijana waliopata ujuzi katika mfumo usio rasmi kurasisha ujuzi huo kuwa katika mfumo rasmi ''Alisema Naibu Waziri Antony Mavunde .

Naibu Waziri Mavunde alisema kuwa katika mpango huo wamiaka mitano utawawezesha vijana wote kuwa nafursa sawa katika soko la ajira baada yakupata ujuzi wafani mbalimbali .
Alisema katika nchi yetu tunayomifumo yakuajiriwa ambayo inamtaka muombaji kazi kuwa naujuzi wa kazi anayo iomba ili aweze kuwajiriwa katika taasisi za umma nabinafsi.
''katika progamu hii tunatarajia kuwafikia vijana milioni 4.4 katika kipindi chamiaka mitano ilikuweza kujiajiri nakuajiriwa ''Aliongeza

Mwenyekiti wa Taasisi binafsi nchini Tpsf Godfrey Simbeye amesema changangamoto iliyopo katika ajira kwavijana nikubwa hali hiyo inawalazimu baadhi yawaajiri kuwachukua vijana wachache katika soko laajira .

Alisema ikilinganishwa nanchi yakenya imepiga hatua katika kukabiliana natatizo hilo baada yanchi hiyo kuamua kuwapa mafunzo maalumu vijana waliopo vyuoni nanje yamfumo waelimu kuweza kupata mafunzo yatakayowezsha vijanawengi kuajiriwa .
''Tuwe nampango mkubwa wakuwawesha vijana ilikuweza kujiriwa na kiajiri wenyewe ''Alisema SIMBEYE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni