Ijumaa, 4 Aprili 2014

DENI LA TAIFA LA ENDELEA KUTIKISA UCHUMI WA TANZANIA YASEMA TCDD

Timothy  Marko.
Deni la ndani  limekuwa likiongezeka kwakiwango hadi kufika asilimia 470 katika kipindi cha  mwezi septemba mwaka 2012 kutoka shilingi bilioni 811.18 hadi kufikia 4624.78 septemba 2012 hali iliyotokanana nakuwepo kwa mtikisiko wakiuchumi nakusababisha serikali kujikita katika soko la madeni ya ndani ilikuwezesha taifa kujikidhi mahitaji yake kifedha.
Akizungumza leo jijini kwenye mkutano waandishi wa habari mkurugenzi mtendaji watasisi ya maendeleo nchini TCDD Hebron Mwakagenda amesema ongezeko ladeni landani lilipewa umuhimu mkubwa  ikilinganishwa na kipindi chanyuma .
‘’katika mwaka 2009 deni la ndani lilikuwa wastani wa asilimia 10 lakini kutokana nakuwepo kwa mgogoro wakiuchumi duniani ulipelekea serikali kujikita zaidi katika soko landani ilikuweza kujikidhi kimahitaji ya kifedha’’alisema Hebron mwakagenda.
Mwakagenda alisema katika kipindi cha mwaka wafedha wa 2008/9 deni hilo landani limendelea kuongezeka kutoka asilimia 16 hadi kufikia asilimia 30 nakufanya ndeni hilo kukua siku hadi siku.
Alisema kuwa hali hiyo imetokana nafedhanyingi kutumika katika kujenga hosteli yamabibo yachuo kikuu cha  Dar es salaam nakuongeza kuwa hali hiyo pia ilitokana nachuo kikuu kuikopa serikali fedha za ndani ilikuweza kujenga hosteli kutoka kwenye mfuko wa hifadhi wa NSSF.
‘’Hali hii imetokana namatumizi ya fedha za ndani ambapo chuo kikuu kili iomba serikali fedha kwajili ya ujenzi wa hosteli ambapo deni hilo lili chukuliwa kutoka chuo kikuu na serikali mwaka2003 nakulipwa February 2012’’aliongeza Mwakagenda .
Hebron Mwakagenda aliongeza kuwa ingawa deni lataifa limekuwa ni dogo ukilinganishwa nala nje lakini limekuwa nariba hali iliyosabababisha  deni hilo kukuwa siku hadi siku.
Aliomgeza kuwa kutokana nahali yadeni hilo kukuwa litafanya na kuleta athari katika uwekezaji wa miundo mbinu nakukwamisha malengo ya millennia kutofikiwa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni