Timothy Marko.
Serikali imepiga marufuku ngoma zinazovunja maadili ya mtanzania ujulikanao kama’’ vigodolo’’nakusimamisha ngomahizo kufanyika mitaani wakati wausiku hali inayochangia kuharibu utamaduni wa mtanzania nakuchochea vitendo vyangono nyakati za usiku .
.Akizungumza leo jijini na waandishi wa habari katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni namichezo Siaba Mkinga amesema ngoma hizo zimepigwa marufuku kufanyika nyakati za usiku kwani imebainika kuwa vitendo vinavyofanyika katika ngomahizozinakiuka maadili ya mtanzania .
‘’sisi kama wizara ya habari utamaduni namichezo tumepiga marufuku ngoma ziitwazo vigodolo ambazo hufanyika nyakati za usiku nakukesha usiku kuchwa hali inayopelekea kufanyika kwa vitendo viovu ikiwemo vitendo vya ngono hali inayochangia ukikwaji wa maadili ya mtanzania ‘’alisema Siaba Mkinga.
Siaba Mkinga alisema kuwa kumekuwa nakushamiri kwa ngoma hizo kwa baadhi yamitaa ya jiji hali inayopelekea kuwepo kwa vitendo vya ngono ambavyo husababisha maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na baadhi ya washiriki wangoma hizo kuji husisha na vitendo vya ngono isiyo salama.
Alisema kuwa katika ngomahizo kumekuwa ikiwahusisha vijana wadogo ambao hujihusisha navitendo vyangono pindi ngoma hizo zinapo chezwa nyakati za usiku hali inayovunja utamaduni wa mtanzania pamoja na maadili ya mtanzania .
‘’ngoma hizi zimekuwa zikiwahusisha hasa vijana wadogo ambao wapo katikaumri wakwenda shule hali inayo changia mmong’onyoko wa maadili kwa vijana hawa napia kujiingiza katika vitendo viovu vya ngono nahata mambukizi ya virusi vyaukimwi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni