WAZIRI WA UJENZI UCHUKUZI NA MAWASILIANO PROFESSA M AKAME MBARAWA akisisitiza jambo wakati akizungumza nawafanyakazi washirika la posta jijini Dar es salaam |
Waziri wa uchukuzi ujenzi na Mawasiliano nchini Professa Makame Mbarawa ameitaka Menejimenti ya shilika la Posta kuweza kuongeza jitihada za makusanyo yatokanayo vyanzo vya mapato vya shirika hilo .
Akizungumza katika kikao cha wafanyakazi pamoja na Menejimenti yashirika hilo jijini Dar es salaamProfessa Makame Mbarawa amesemakuwa shilika hilo linavyanzovingi vya mapato ambavyo vikikitumiwa kwa usahihi vitaweza kulisaidia shirikahilo kujikwamua kiuchumi .
''Mmekuwa mkililia serikali iweze kuwasaidia lakini niwaambie uwazi kuwa shida yenu sio fedha bali shida yenu niuongozi bora kwani mimekuwa nauzoefu katika shirika la reli lilikuwa namigogoro kama mliokuwa nayo ninyi lakini mara baada yakubadilisha uongozi sasahivi TRL Mambo yapo safi''Alisema waziri Makame Mbarawa.
Professa Mbarawa alisema kuwa atahakikisha shirika hilo linapata kiongozi sahihi na aliyekuwa nasifa mwenye uwezo wakuliendesha shirika hilo kibiashara ilikuweza kulieletea shirika mapato pamoja nataifa kwa ujumla ili shirika hilo kuweza kuendelea kuwa kitovu cha mapato yaserikali yatokanayo huduma zitolewazo katika shirika hilo
.
Alisema kuwa moja yakazi yakiongozi huyo nikuwaletea shirikahilo kiongozi atakaye dumisha maslahi nchi nataifa kwaujumla nasio kiongozi atakayekuwa mtafunaji fedha kupitia shirika hilo nakuwataka wafanyakazi wawe nasubira nakuweza kudumisha ushirikiano kwakiongozi huyo.
''nitawaletea kiongozi ambaye halijui kabisa shirika laposta lakini anaweza kuliongoza shilika hili la posta hivyo kikubwa zaidi ninawtaka wafanyakazi washirika hili kufanya kazi ili kuliletea tija taifa hasa kiuchumi kwani shirika hili lina mali nyingi ambazo zikitumiwa vizuri zina weza kulisaidia shirika ''Aliongeza WAZIRI waujenzi uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa.
Naye Mwenyekiti wa bodi wa shilika hiloDK. Haruni Kondo alitoa ahadi yake kwa waziri huyo kuwa yeye nabodi yake itaendelea kushirikiana nawizara hiyo ilikuweza kufanya kazi kwa ufanisi na kwauaminifu .
Alisema kuwa shirika hilo linalenga kuwa kipaumbele katika makusanyo ya vyanzo vya mapato vya shirika hilo nakuahidi kuwa shirika hilo litakuwa nishirika lenye hadhi kitaifa nakimataifa .
''sisi tunataka kuwa viumbe bora tunataka tuifanye shirika laposta nchini kuwa nlenye heshima nchini nabodi hii ambayo umeichagua tutahakikisha tunafanya kazi kwa ufanisi zaidi'' Alisema Dk.harun KONDO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni