Alhamisi, 26 Januari 2017

WAANDISHI WA HABARI WAONYWA KUTUMIA PROPAGANDA NA UMOJA WA MATAIFA .

Tokeo la picha la STELA VUZO
MUWAKILISHI MKAAZI ,MSEMAJI WA UMOJA WA MATAIFA STELA VUZO AKIZUNGUMZA NA WANAHABARI
Timothy Marko.
WAKATI Dunia ikiadhimisha siku ya Mauaji ya Horicust yaliolengwa kuwaua Wayahudi milioni sita yaliyofanywa Dikteta Adolf Hitler kupitia Chama cha Nazi cha Ujerumani Mwaka 1939,Jamii nchini pamoja nawanasiasa nchini wameaswa kutoeneza Propaganda zitakazochochea chuki baina jamii hizo ilikuepukana na madhara makubwa kama yaliyo tokea nchini Ujerumani january 27, 1939 .

Hayo yamebainishwa na Muwakilishi Mkaazi wa ubalozi wa ujerumani Susan Keller wakati wamaadhimisho yakumbukumbu ya Athari yavita yapili yadunia iliyochochewa na Diktekta Adolf Hitler jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa vitendo vingi vya chuki dhidi ya wayahudi vilivyofanywa na wajerumani vilichochewa na Waandishi wa Habari walioneza chuki dhidi ya wayahudi .

''Tunaona sababu kubwa yavita yapili vyadunia vilichochewa na waandishi wa habari waandishi wa habari wengi walitumia propaganda za chuki dhidi ya wayahudi nakuweza kusababisha vifo vipatavyo milioni sita ''Alisema Susan Keller .

Keller alisema kuwa madhara yavita pili yadunia yameweza kuonekana hasa katika nchi yaujerumani kwani hapo awali yalisababisha baadhi ya wananchi wa nchi hiyo kukosa elimu na kutoweza kufanyakazi hali iliyochangiwa napropaganda za wanasiasa .
Alisema kuwa propaganda nyingi ziliweza kuibuliwa nawaandishi wa habari kwakutumia mashapisho mbalimbali napicha ambazo zilileta uhasama mkubwa na wayahudi .
''Vyombo vingi nchini ujerumani viliweza kuchochea mauaji yawayahudi hali iliyocha gizwa na machapisho mbalimbali ikiwemo magazeti na vyombo vya runinga ,nilazima dunia tujiadhari na wanasisa nwanoleta siasa za chuki zinzotokana na propaganda ''Aliongeza Keller.

Naye Msemaji wa tawi la Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Stella Vuzo amesema kuwa Mauaji ya wayahudi yaliyofanywa na wajerumani chini ya utawala wa adolf hilter yalifanywa kwa kutumia moto .
Alisema tukio hilo lililenga wayahudi tu hii nikutokana wajerumani kuwa nahofu ya wayahudi kumiliki sehemu mbalimbali za uchumi ambapo takribani watu 6000000 waliuwa na milioni 55 ambao siwayahudi wa lipoteza maisha .
''KITENGO hiki cha uelimishaji chini ya umoja wa mataifa tunakumbuka sana tukio hili ambalo lilitokea january 27 1939 lakini Tanzania tumeamua kuadhimisha leo kwasababu maalumu''Alisema Stella VUZO .
Vuzo alisema kuwa mauaji hayo ya  horicust yalilenga ubaguzi dhidi ya wa yahudi ambapo vitendo kama hivi vinapingwa na umoja wa mataifa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni