Jumatano, 25 Januari 2017

WANANCHI WAASWA KUNUNUA HISA KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

Tokeo la picha la aloys MWAMANGA
Mwenyekiti wa BODI ya TCCIA Mhandisi Aloyce MWAMANGA


Timothy Marko .

WANANCHI wameaswa kununua hisa ilikuwekeza katika sekta ya viwanda ilikuwezesha sekta hiyo kuweza kujenga uchumi ilikuweza kuondokana na umasikini nakuweza kufika nchi zenye uchumi wa kati ifikapo 2025.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya TCCIA Mhandisi Aloyce Mwamanga mapema hii leo jijijini Dar es salaam  Katika mkutano wa uhamasishaji wa ununuzi wa hisa katika kampuni hiyo ambapo amesema kuwa jumla ya hisa zenye thamani milioni 45 zinatarajiwa kuwekezwa ilkuweza kukamilisha ujenzi wa majengo yakisasa katika mikoa ya Dodoma na Mtwara .
''Kumekuwa na uelewa mdogo juu ya uwekezaji kupitia hisa kwa makapuni mbalimbali kwa wananchi nilazima mamlaka zilizopo ziwezinatoa elimu endelevu kuhusiana na uwekezaji katika hisa ili kuweza kujenga uchumi ''Alisema Mhandisi Aloyce Mwamanga .

Mhandisi Mwamanga amesema kuwa kufuatia sheria 2002 ya fedha juu ya uwekezaji unazitaka taasisi zote kuweza kutoa taarifa kwa wananchi ilikuweza kufahamu masuala mbalimbali ya uwekezaji ili kujenga uchumi nakuweza kujiletea maendeleo .
Amesema Kuwa Tangu Kampuni hiyo ianze shughuli zake imejiorodhesha katika soko lahisa la Dar es salaam ilikuweza kupanua vyanzo vyake vya mapato ilikuweza kupunguza athari za kutegemea chanzo kimoja tu cha mapato .

''Kupitia zoezi hili kampuni itaweza kutoa fursa kwa wanahisa kuongeza hisa zao na pia kuwezesha wananchi wengine kuwekeza kwenye kampuni yetu ''Aliongeza .
Katika hatua nyingine Naibu Katibu MKUU wa wizara Fedha nauchumi Doroth Mwanyika amipongeza bodi hiyo nasoko lahisa Dar es salaam kwajuhudi zake zakukuza ushiriki wa watanzania kumiliki uchumi .
Mwanyika amesema kuwa nanawapongeza watanzania wengi kujitokeza katika kuchangamkia fursa mbalimali katika kujnga uchumi .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni