JESHI la polisi kanda maalum jijini Dar es salaam limepiga marufuku wafanyabiashara wanaouza visu ,mishale majambia pamoja namapanga hadharani pasipokuwa nakibali cha jeshi hilo .
Akizungumza na waandishi wa habari Kamishina wa polisi wa kanda hiyo Simon Sirro amesema hatua hiyo yakupiga marufuku uzwaji wabidhaa hizo imetokana baadhi ya watu wasio waaminifu kutumia silaha hizo kufanya uhalifu ikiwemo unyang'anyi.
''kuaanzialeo hatu taki biashara ya visu mishale pamoja mapanga barabarani ukitaka kuuza bidhaa hizi lazima uwenaleseni maalum''Alisema Kamishina Simon Sirro.
Kamishina Sirro amesema kuwa sambamba nakupiga marufuku uzwaji wa mishale pamoja na mapanga pia ameweza kupiga marufuku uuzwaji wa manati barabarani.
Katika hatua nyingine jeshi hilo linatarajia kuadhimisha siku ya polisi kuanzia kesho ambapo maadhimiasho hayo yanatarajiwa kuhudhuriliwa na waziri wa mambo yandani Mwigulu Lameck Nchemba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni