Jumatano, 11 Januari 2017

DIAMOND KUIPEPERUSHA TANZANIA AFCONw

WAZIRI WA HABARI, SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI NAPE NNAUYE AKIZUNGUMZA NA WANAHABRI (HAWAPO PICHANI) JUU YA UFUNGUZI WA MICHUONI YA AFCON.

MSANII DIAMOND PLATMAN AKIKABIDHIW BENDERA YA TAIFA NA WAZIRI NAPE NNAUYE.
Timoth Marko
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ‘Bongo fraver’ Nasibu Abdul (Diamond) amechaguliwa kuwa mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza katika ufunguzi wa mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON -2017)
Akizungumza na wanahabari jijini Dar Es Salaam mapema leo, mkurugenzi mtendaji wa Multchoice Tanzania Salum Salum amesema; hatua ya kuchaguliwa kwa Diamond miongoni mwa wasanii walioteuliwa kutumbuiza katika hafla hiyo inachukuliwa kama fursa kwa Tanzania kusikika zaidi katika mashinda hayo japokuwa timu ya Taifa Stars ya Tanzania haikuweza kufunzu matima mashindano hayo.
 “DStv ndicho king’amuzi kitakachoonyesha michuano hiyo mubashara inayotarajiwa kuanza hivi karibuni kupitia suparspot4 (DStv 204) ili kuwawezesha watanzania wengi zaidi kuiona michuano hiyo moja kwa moja” alisema Salum Salum.
Pamoja na hayo ametanabaisha kuwa michuano ya AFCON yam waka huu inanogeshwa zaidi kwa kuwepo wachezaji nguli wa mpira wa miguu duniani wanaochezea vilabu vikubwa dunia mfano, Alsenal, Chersea na nyinginezo.
Wakati huo huo Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema kuwa kuwepo kwa msanii huyo wa kizazi kipya Diamond katika mashindano ya AFCON ni hatua kubwa ya kujivunia na kwamba serikali imeahidi kumpa ushirikiano sambamba na kampuni ya Multchoice Tanzania.
“serikali itapitia sheria zenye mapungufu kabla ya bunge la lijalo halijaanza kuweza kuangalia wapi parekebishwe ili kuangalia sehemu zilizo katika sheria hiyo ambazo zimekuwa ni kikwazo katika sekta binafsi” alisema Waziri Nape Nnauye.

Msanii Nassib Abdul ‘Diamond’ ameishukuru serikali kwa mchango wake katika kufanikisha safari yake ya kuelekea Gabon na amewaahidi watanzania kuwa aendi kama kundi la WCB ila anenda kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano hayo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni