Ijumaa, 13 Januari 2017

TUME YA UCHAGUZI YAVITAKA VYAMA VYA SIASA KUWASILISHA MALALAMIKIKO YAO.

 Tokeo la picha la ramadhani kailima
Timothy Marko.
TUME ya uchaguzi nchini (Nec)imevitaka vyama vya siasa nchini kuwasilisha malalamiko yao juu ya mwenendo wauchaguzi mdogo uliofanyika katika kata ishirini za Tanzania bara hivi karibuni .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo Ramadhani Kailima amesema kuwa uchaguzi huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi sehemu ya 5.3 ya maadiliya uchaguzi wa Rais wa bunge na madiwani ya mwaka 2015ambayo yalisainiwa na tume ya uchaguzi.

''Tume ya uchaguzi inavitaka vyama vyasiasa ,wagombea wanaoamini kuwa maadili ya uchaguzi yamekiukwa awasilishe malalamiko yake katika kamati ya maadili ya ngazi husika ''Alisema Mkurugenzi wa uchaguzi Ramadhani Kailima .

Mkurugenzi Kailima alisema kuwa kutokana kuwepo kwa malalamiko kutoka katika chama cha ACT wazalendo kulalamikia tume hiyo juu yautaratibu kukiukwa katika mchakato wa uchaguzi mdog,tume hiyo inakitaka chama hicho kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa maadili katika kamati husika .

Alisema kutokana sheria ya maadili sehemu 5.4 ya maadili yauchaguzi inwataka kuwasilisha malamiko hayo juu ya ukiukwaji wa sheria za uchguzi kwa muda usiopungua masaa 72 tangu ukiukwaji wa sheria umeweza kufanyika .

''Iwapo chama cha siasa au mgombea hataridhidhika na maamuziya kamati ya maadili ngazi ya kata kwakuzingatia sehemu ya 5.7(a)ya maadili yauchaguzi awasilishe rufaa kwa msimamizi wa uchaguzi ngazi yajimbo ndani ya saa 24tangu maamuzi kamati yamaadili yalipo tolewa''aliongeza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni