Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Luhaga MPINA |
TimothyMark
KUFUATIA kuwepo kwa baadhi ya viwanda vilivyopo katika
kata ya changombe nakudaiwa kutitirisha maji taka katika mtaa keko keko
magurumbasi B jijini Dar es salaam , Naibu waziri wa Mazingira ofisi ya makamu
wa Rais Muungano na mazingira Luhaga
Mpina amewapa mwezi mojaTanroad kuhakisha
wanajenga bomba litakalo tumika kupitisha maji hayo.
Akizungumza katika ziara yake yakushitukiza katika eneo
hilo Mapema hiileo jijini Dar es Salaaam,Naibu waziri Mpina amesema viwanda
vyote vitakavyobanika kutirisha maji vitachukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa
kuendelea nashughuli za uzalishaji.
‘’Ninawashukuru sana ,nimeshuhudia mambo haya hayawezi
kuvumilika kwanzia sasa ninatoa mwezi
moja kuhakisha wanajenga bomba moja litakalo tirisha maji namambo haya yasijirudie
tena ‘’Alisema Naibu Waziri luhaga Mpina .
Naibu Waziri wa mazingira ofisi ya makamu Rais Mpina
amesema kuwaviwanda katika eneo hilo vitakavyodaiwa kutirisha maji taka bila
kuzingatia kanuni za mazingira katika maeneo yao vitachukuliwa hatua ya kisheria.
Alisema kuanzia leo viwandahivyo vinatakiwa kusitisha
shughulizake mpaka ujenzi wabomba maalumu lakutoka dwasco liwelimekamilika .
‘’Wenye viwanda viwanda vinavyotirisha maji pasipo
kuzingatia kanuni za kimazingira wajiandae,ninasitisha shugulizote za
viwanda sehemu hii mbaka ujenzi wa bomba
maalumu utakapo kamilika lakutoka dawasco hatuwezi kuvumilia hali
hii’’Aliongeza naibu waziri Mpina.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Keko MagurumbasiHendudary Sabu amesema kuwa baadhi ya viwanda hivyo vimekuwa
natabia yakutirisha maji taka bila kuzingatia kanuni za kimazingira kwa muda
mrefu.
Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha kwa watoto wadogo
kuchezea maji yenye sumu nakubabuka katika mili yao nakutoweza kupata fidia
yeyote kupitia viwanda hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni