Jumatano, 21 Desemba 2016

JESHI LAPOLISI KUENDELA NAUCHUNGUZI WA KADA WA CHADEMA .

Tokeo la picha la ROBERT BOAZI
KAIMU Mkurugenzi WA UPELELEZI  MAKOSA YA JINAI CP ROBERT BOAZI
TimothyMarko.
JESHI lapolisi nchini limesema kuwalinaendelea kufanya uchunguzi juu ya kupotea Mwanachama wa chadema anajulikana Benard Focus Maarufu Beni Saanane baada ya hivi karibuni Mwanasheria wa chama hicho Tundu Lisu kulitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya mtu huyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa Makosa yajinai Cp Robert Boazi amesema kuwa jeshi hilo lilipata taarifa za kupotea kwa mwanachama huyo wachadema kwaliyejitambulisha kuwa nirafiki yake .
''Baada ya kupokea taarifa za jalada la uchunguzi nakufuatwa kwa taratibu zote zakufungua jalada lake taaraibu zinaendela za kiupelelezi juu yakupotea mtu huyo katika mazingira ya kutatanisha ''Alisema Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Cp Robert Boazi.

Kamishina Wa Polisi Boazi alisema kuwa endapo mtu yoyote atakuwa nataarifa za kupotea kada huyo wachadema atoe taarifa kwajeshi hilo ili jeshi hilo liweze kuzifanyia kazi taarifa hizo .

Alisema wakati jeshi hilo linafanya uchunguzi jeshi lapolisi nchini limewataka kuwa watulivu jeshi hilo limewahaidi wananchi kutoa taarifa juu ya kada huyo wa chadema .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni