Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita |
Timothy Marko .
Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewataka mawakala wa maegesho katika jiji hilo kuweza kuvaa sare sambamba nakuwa nakitambulisho kinachowatambulisha mawakala maegesho pamoja nakuwataka kuhakikisha wanakuwa na mashine za EFd ilikuweza kukusanya mapato ipasavyo ya jiji hilo.
Kauli hiyo ameitoa mapema hii leo katika ukumbi wa Karimjee jiijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kero zinzodaiwa kufanywa na mawakala hao wakiwa katika majukumu yao .
''Wakala anatakiwa kuvaa sare na sambamba nakitabulisho cha kazi ,sambamba nahili wakala anatakiwa kuwa namashine za EletronicFiscaldevice (Efd )ambazo zinatoa risiti zenye muhuri wa Manispaa''Alisema Meya Isaya Mwita .
Mwita alisema kuwa atafanya ukaguzi juu ya utekelezaji wa maagizo hayo ifikapo january Mosi mwakani nakuwataka wananchi kuwa makini kwawatu ambao wanatoa Huduma ya maegesho pasikuwa na risiti.
Alisema endapo mtoa huduma atabainika anatoa huduma ya maegesho pasipokuwa narisiti pamoja na Efd mtoa huduma hiyo atafikishwa katika vyombo vya sheria nakufutiwa leseni yausajili.
''HADI sasa tunazo mashine za kutosha zipatazo 875 za efd kwahiyo tunawaomba wanachi kuweza kudai risiti mara wanapotumia huduma yamaegesho zilizoidhinishwa na TRA ''Aliongeza Isaya mwita
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni