MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MAPEMA HII LEO. |
KATIKA kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa ikiwemo Migogoro ya Ardhi katika jiji la Dar es salaam,Mkuu wa mkoa wa jiji hilo Paul Makonda ameliteua jopo la Wanasheria wapatao 35 ili kuweza kutatua kero mbalimbali za migogoro ya ardhi.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amesema kuwa uteuzi huo wa Wanasheria unaendana sambamba nautatuzi wa kero mbalimbali katika manispaa zilizopo katikajiji hilo kwa kushirikiana na wakuu wawilaya wamanispaa hizo .
''Sisi tunafarijika sana hasa vijana wanavyotupa moyo ,kutokana nawanasheria wengi waliohapa takribani35 tunawatuma kwalengo mojatu waende katikawilaya za jiji la Dar es salaam wakatatatue migogoro yaardhi ambayo imekuwa nikero kwa wanachi kama agizo la Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DK.JONH POMBE Magufuli yakutaka kero za wananchi zinatatuliwa ''Alisema Mkuu wa mkoa PAUL Makonda .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Makonda alisema kuwa nilazima wanasheria hao kuweza kuzingatia maadili wakati wautendaji wao wanapo tatua migogoro ya aridhi nakuepukana navitendo vya Rushwa .
Alisema lengo lakuwateua wanasheria hao sio kujaza fedha katika mifuko yao nabadala yake kuhakikisha migogoro ya ardhi pamoja namirathi inatoweka kabisa nakukoma katika jiji hilo .
''Ningefurahi sana kama ningepata matokeo chanya yakuhusiana namigogoro ya ardhi na matokeo chanya kuhusu mirathi katika jiji letu kwani migogoro hii imekuwa nikero kwa wananchi ,ninataka ufaulu wenu usiwe kwenye makaratasi tu bali ufaulu wenu uwe kwavitendo ''Aliongeza Paul Makonda .
Makonda aliongeza kuwa wanachi wengi wamekuwa wakilalamika juu ya ucheleweshaji wakesi hasa katika ardhi ,nakuwataka wanasheria hao wawe mwarobaini wa ucheleweshaji wakesi hususan katika ardhi .
KATIKA hatua nyingine Mkuu wamkoa huyo alitoa mgawanyo wa wanashaeria watakaosimama kama mwarobani katika utatuzi wamigogoro ya ardhi na mirathi aliwataja wanasheria katikawilaya ya kinondoni tisa ubungo na ilala kumi nambili wakati wilaya kigamboni sita huku Temeke Wanasheria wanne watakao tatua migogoro hiyo.
Naye Mkuu wa wilaya wa Temeke Felix Lyaniva amesema kuwa uteuzi wa wanasheria hao umekuja wakati muafaka kufuatia kauli ya Rais wa JAMUHURI ya muungano Wa Tanzania Dk.JONH pombe Magufuli lakuwatetea wanyonge .
Alisema kuwa kumekuwa nachangamoto kubwa kwa wananchi juu ya uelewa washeria hali inayochangia ucheleweshaji wa kesi Mahakamani .
''kumekuwa na changamoto ya uelewa wa washeria kwa baadhi ya wananchi hali inayopelekea ucheleweshaji wakesi mahakanani ,utakuta waajiri wengi wamekuwa wakiwafukuza wa ajiri wao napia suala lamigogoro ya ardhi nikubwa nimefurahi kupewa wanasheria hawa ''AliSEMA Lyaniva.
kwaupande wake Muwakilishi wa wanasheria hao Georgia Kamina amesema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwakuweza kuwaamini vijana nakuweza kumuahidi Rais MAGUFULI watafanya kazi hiyo kwa uaminifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni