Na Leonard Mutani
Usafiri
ni sehemu mojawapo ya kujongea kutoka sehemu moja na kuelekea sehemu
nyingine huku chombo chochote kinachoweza kukusafirisha sehemu husika
kwa lengo linalofanya kwenda hapo, hii ni sehemu ya maisha ya binadamu
inayofanya neno usafiri kuwepo kwenye mfumo mzima wa maisha ya kila
siku.
Mfano wa Safari za mwanzo kabisa kusafiri hapa Africa.
|
Hii inatokana na binadamu kukaa na kutafakari nini kifanyike kupunguza urasimu wa kupoteza muda wa kutembea, hata hivyo pamoja na kuwepo kwa mazingira ya kupunguza muda wa mtu kutoka eneo moja mpaka lingine, teknolojia ilileta chombo kijulikanacho kama pikipiki ya magurudumu mawili, hiki ni chombo kilichokuja kusaidia kupunguza muda na kuharakisha safari, kwa nchi za kiafrika imekuwa ni msaada mkubwa ikiwa na maana hata kule chombo kingine kisipoweza kufika kutokana na njia, ufinyu wa eneo pamoja na gharama, basi chombo hiki kinaweza kufika kwa wakati na kwa garama ya chini.
Hii ni baada ya harusi, safari inaanza.
|
Hata
hivyo uwepo wa chombo hiki hususani hapa nchini umekuwa na faida na
hasara zake kutokana na matumizi yanayotumika tofauti na watengenezaji
wake hama sheria za nchi kinapotumika.
Hapa
nchini kumekuwa na baadhi ya waendesha pikipiki hizo maarufu (Bodaboda)
wakitumia chombo hicho tofauti na uwiano mahususi, kutokana na hilo
waendeshaji wengi hama abilia waliowahi kubebwa wamebaki hawana moja ya
kiungo cha mwili kutokana na ajali iliyotokea kutokana na kutofuata
utaratibu unaopaswa, hivyo kupelekea makosa na maumivu kwa mhusika.
Hapa chini tumekuwekea picha
kadhaa zikionyesha moja matumizi yasiyo sahihi kwa pikipiki ya
magurudumu mawili iliyoweza kubeba abilia na muendeshaji wake kufikia
watu sita (6), hapo ni eneo la Mbagara Kisewe, ambapo ilipouliza kwa
vijana wengine ambao walishuhudia hali hiyo tulipata hili hapa,
“kaka hali
hii sisi wenyewe hatuipendi ila inatokana na abilia mwenyewe anakuja na
wenzanke kama unavyoona anakwambia tunaenda sehemu fulani tuna shs
1000/- ukiangalia bosi anasubili hesabu na sehemu wanapokwenda siyo
mbali basi unawapelekea hivyo hivyo tu” alisema Mohamed mmoja wa waendeshaji wa bodaboda wa eneo hilo.
Hii ni pikipiki inayoruhusiwa kubeba watu wawili lakini hapa imeweza kubeba watu sita kwa mara moja kitu ambacho si kawaida.
|
Mpita
njia akipita karibu na pikipiki iliyobeba watu sita, kupitia picha hii
ndipo unaweza kuwaona wote waliobebwa, mbele ni (1) kijana mdogo,
anayefuatia ni (2) dereva wa pikipiki hiyo, nyuma yake kuna (3) binti
mdogo kavaa ushungi wa bluu,anayefuatia (4) mwenye kilemba cha njano
kuna (5) mtoto wa kike anaonekana kichwa ambapo wa mwisho ni (6) dada
mwenye ushungi mwekundu na ameshika kikapu.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni