MWANASHERIA WA CHADEMA TUNDU LISU |
CHAMA cha demokrasia na Maendeleo nchini (CHADEMA)kimelitaka jeshi la polisi nchini kuweza kufanya uchunguzi wakina yajuu yakuondokewa namwanachama wachama hicho ajulikanaye kama Benson Saanane baada ya chama hicho kudai hawana taarifa mahala alipo mwanachama huyo.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika makao makuu yachama hicho mapema hii leo jijini Dar es salaam Mwanasheria wa Chama hicho Tundu lisu amsema kuwa awali mwanachama huyo alionekana katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa afrika Mashariki naspika wa bunge lasita Samweli Sitta .
''Beni Saanane Mara yamwisho aliweza kuonekana katika mazishi ya Samweli sitta November 14 mwaka huu baada yahapo hakuwa anatembea namwenyekiti wetu wa chama tangia hapo hakuwa na mwenyekiti wachama hadi mwenyekiti aliposafiri katikashughuli za chama nchini uingereza nakumaliza ziara yake ujerumani ''Alisema Mwanasheria Tundulisu .
Mwanasheria wa Chadema Tundulisu alisema kuwa Serikali inawajibu wakulinda Raia wake kwani hata yeye pamoja nachama chake hawa fahamu kuwa mwanachama wachama hicho ama yupo hai au amekufa .
Alisema hata walipotaka kupata taarifa kutoka kwa nduguzake mwanachama huyo walidaikuwa ndugu yao hawafamu alipo ,nakuiomba jeshi lapolisi kuweza kufanya uchunguzi juu ya utata wa mwanachama huyo.
''Vyombo vya usalama vituambie Benisana yupo wapi kwani serikali inaouwezo wakunukuu mawasiliano ya beni sanane nakujiua wapi alipo ,serikali ndio inadhibiti mipaka yetu baharini na nchi kavu naomba serikali ituambie amekwenda wapi! ''Aliongeza Mwanasheria huyo.
Aliongeza kuwa hivi karibuni Mwanachama huyo aliwezakupokea meseji za vitisho kutoka kwamtu asiyefamika akiwa na namba 0768797982 ikimuonya kuwa anacho kitafuta atakipata .
Bensonsanane amekuwa akidaiwa kutoa lugha za kashifa juu ya serikali ya awamu yatano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni