WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TENKNOLOJIA PROFESA JOYCE NDALICHAKO . |
WAZIRI wa Elimu,Sayansi ,na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka Wadau wa Sekta ya Elimu nchini kuweza kuwakumbusha vijana juu kuzingatia Maadili na kuondokana na vitendo vya rushwa ilikujenga jamii yenye Maadili nchini .
Akizungumza katika Mdahalo wa kukuza nakujenga maadili mapema hii leo jijini Dar es Salaam Waziri Ndalichako amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatetea watoto wao pindi wa napokutwa nauvunjifu wamaadili hali inayochangia kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mmongo'nyoko wa madili kwa vijana .
''Kumekuwa na Baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatetea vijana wao pindi wa napotenda makosa na kuadhibiwa nawalimu mashuleni hali inayochangia uvunjifu wa maadili kwa vijana ,ili kurejesha Maadili kwa vijana nilazima elimu yauraia itolewe kwa vijana ilikuondokana na kasi ya utumiaji wa mitandao ambayo mingi imekuwa ndio chanzo cha uvunjifu wa maadili ''Alisema Waziri wa Elimu Professa Ndalichako .
Waziri Ndalichako alisema kuwa Suala la Maadili nisuala Muhimu katika Makuzi ya Vijana ambayo inanalenga kumtambulisha mtu kwenye jamii yake nakuwa kielelezo muhimu chakupima Maadili ndani jamii .
Alisema kuwa Msingi Mkubwa wa Maadili unajengwa ndani ya familia ambapo baadhi ya vijana wanatokea katika familia hizo nakuwataka wavijana hao kuweza kuiga matendo mema na kuepuka vitendo viovu nakuwataka vijana hao kuwa wasikivu kwa wazazi wao .
''Mnatakiwa kuzingatia matendo Mema epukeni Matendo Maovu na hakikisheni muda wote mnakuwa wasikivu na mnaofundishika ''Aliongeza Waziri Ndalichako.
Katika hatua Nyingine Mkurugenzi wa Taasisi ya kudhibiti na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU ) Vallentino Mlowa amesema kuwa ili jamii iweze kuwa na maadili ielimishwe juu ya umuhimu yakuwa na maadili mema katika jamii .
Mlowa Alisema kuwa nivyema Wizara nataasisi hiyo kukuweza kukaa pamoja ilkuweza kujenga mitaala itakayo jenga jamii iliyo bora .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni