MKURUGENZI WA OFISI YA TAKWIMU,DR Albina Chuwa
Timothy Marko.
Timothy Marko.
WADAU wa sekta ya takwimu nchini wametakiwa kutopotosha
taarifa za takwimu wanazopewa kwani taarifa hizo ni nyenzo muhimu katika ukuaji
wa uchumi na kufikia Dira ya maendeleo ya mwaka2025.
Akizungumza katika uzinduzi wa siku ya takwimu Barani Afrika
mkufunzi wa chuo cha Afrika cha Takwimu nchini, Dk.Kasala Camilius amesema kuwa
wakati Dunia ikielekea katika malengo 17 endelevu ya millennia kati ya malengo manane yanagusa sekta hiyo, lazima wadau hao kuweza
kuzingatia weledi waukusanyaji Takwimu
’’ilikuweza na kuakikisha malengo ya millennia
yanafanikiwa tunapaswa kuwa na wataalamu wa
taaluma rasmi ya takwimu watakao weza kukusanya takwimu kwa kuzingatia
vigezo kumi ambapo moja ya vigezo hivyo ni pamoja na kuwa na takwimu zitakazo
zingatia vigezo pamoja na viwango sambamba na takwimu zinazo zingatia uadilifu
wa taaluma ya Takwimu nchini.’’ Alisema Dr. kasala
Aidha Dr. kasala ameongeza kuwa ili
viongozi wa Afrika kuweza kufikia malengo yao ya millennia ya mwaka 2063 ni
lazima kuwepo na takwimu sahihi zitakazo chochea mipango ya maendeleo ili kuondokana
na tatizo la umaskini.
Amesema ili kuweza kupata matokeo
bora ya utafiti wa takwimu mbalimbali ni lazima Data zinazo tolewa ziwe bora
kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo njia ya Tehama ili kuweza kufanya uchambuzi
.
Kwa upande wake naibu Waziri wa AFya
jinsia Wazee na Watoto Dr. Hamisi kigwangala amesema kuwa ni vema wadau wa
takwimu kuwekeza muda wao katika kufanya tafiti za Takwimu za kiuchumi ili
kuiwezesha Serikali kufanya mipango ya maendeleo.
Amesema kuwa Serikali haina budi kutumia Takwimu zilizo thibitishwa
kitaalamu na kuondokana na Takwimu ambazo hazijathibitishwa.
‘’Sisi kama Serikali hatuwezi kutumia
Takwimu za ovyo ovyo lazima tutumie Takwimu zilizo thibitishwa na taasisi kama
COSTECH,udhibiti wa taarita za ovyo ovyo lazima ufanyiwe uchunguzi na Taasisi
hii ili kuiwezesha Serikali kupata Takwimu sahihi,’’Alisema Kingwangala
Katika hatua nyingine mkurugenzi wa
Ofisi ya Takwimu Nchini Dr. Albina Chuwa amesema kuwa Taasisi yoyote inayo
fanya Takwimu nilazima kutoa ushirikiano wa Taasisi nyingine katika zoezi la
ukusanyaji wa Takwimu ili kuweza kupata Takwimu sahihi.
Aidha lisema kuwa ni vema wadau waTakwimu
nchini wanapokusanya Takwimu kufuata
misingi ya kutambulika na Tasisi kama COTSECH, ili kuondokana na tatizo la
upotoshwaji wa taarifa ambazo ni chachu ya maendeleo nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni