Blogu hii makini iko kwa ajili ya kuhabarisha masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Karibuni sana.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Ali Salum Hapi ametoa tahadhari kwa wahusika waliofanya ubadhilifu
katika kuwapatia pesa za misaada ya Tasaf kwa wasiostahiki na
kusababisha upotevu wa fedha za serikali. Hayo ameyasema leo katika
mkutano wake na Waandishi wa Habari akidai kuwa wote waliopata fedha
hizo wanatakiwa wazirudishe mahala stahiki ili zifanyiwe kazi kwa
wanaostahiki.
Hapi amesema Tasaf na pesa
zilizotolewa zilikuwa kwa ajili ya kuwasaidia kaya zilizo na hali mbaya
kiuchumi ili ziwasaidie kupata nguo za shule pamoja na huduma nyingine
za kijamii, hivyo udanganyifu uliofanyika umebaini kaya hewa 566 pia
kaya nyingine 265 na kaya nyingine 59 zote za Wilaya ya Kinondoni pamoja
na kaya zilizobaki wamehama maeneo hayo hivyo kuna fedha zinachukuliwa
na haijulikani wapi zinaenda baada ya kubaini na kufanya uchunguzi wa
fedha hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni