Alhamisi, 22 Septemba 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA APOKEA ZAIDI SHILINGI MILIONI 200 KUWAHUDUMIA WAKAZI WA MKOA WAKAGERA

Tokeo la picha la waziri mkuu

WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA KASIMU MAJALIWA



Timothy Marko.
WAZIRI MKUU Kasimu Majaliwa leo amepokea misaada mbalimbali yakijamii yenye thamani ya shilingi milioni 200,kwajili yawahanga watetemeko la ardhi liliotokea huko Mkoani Kagera
 .
Misada hiyo yenye thamani milioni 200 imetolewa  katika ofisi yawaziri mkuu ambapo jumla yataasisi zisizo za kiserikali zipatazo sita zimemkabidhi vifaa ikiwemo chakula na mifuko ya cement tani 40 kutoka katika kamupuni inayojishughulisha na ujenzi ya Advert Construction .

‘’Baadhi ya makapuni yaliyojitokeza ni kutoka kwenye Group la Amadia ambapo wameweza kutoa shilingi milioni 4 na vifaa tasilimu vyenye thamani ya milioni sita sawa na shilingi milioni kumi ‘’Alisema WAZIRI MKUU Kasimu Majaliwa .

Waziri Mkuu Majaliwa aliyataja makampuni mengine, kampuni ya ujenzi ya advert Construction ambapo yameweza kutoa tani 40 ambapo meneja wa kampuni hiyo tayari ameshawakilisha tani hizo za simenti mjini Bukoba.

Alisema Sambamba na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ambapo meneja wa kampuni hiyo aliahidi kutoa vifaa vya mawasiliano kusaidia sekta yaelimu pamoja na hundi yamilioni 100.

‘’Mfuko wa pesheni LPF Tayari umeshawasilisha hundi yamilioni milioni 20 wakati taasisi international art living imeweza kuchangia vifaa vya milioni 10 ikiwemo unga na mchele ‘’aliongeza 
.
KATIKA hatua nyingine Waziri mkuu Majaliwa ametoa pongezi kubwa kutoka kwenye makapuni hayo kutoa msaada huo aidha amehaidi kuwashukuru wadau hao kwanjia yamaandishi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni