AFISA UHUSIANO WA MFUKO WA PENSHENI WA PPF LULU MENGELE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA ZOEZI LA UHAKIKI WA WASTAAFU NCHINI . |
Timothy Marko.
MFUKO wa Pensheni
nchini (PPF)unatarajia kuendelea na
uhakiki wa wastaafu kuanzia Jumatatu
ijayo katika mikoa ya kanda Mashariki na
kati, Morogoro ,Dodoma na Singida .
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Meneja Kiongozi wa
Pensheni na Huduma, John Mwalisu,amesema kuwa uhakiki huo unaendelea mikoa
mingine baada ya kumalizika Dar es Salaam.
‘’Uhakiki
wamikoa mingine ya wastaafu nipamoja na Kanda ya ziwa katika mikoa ya Mwanza
,Mara ,Kagera ,kigoma mjini ,shinyanga mjini ,Tabora mjini Geita mjini ,Simiyumjini ,Maswa pamoja na mkoa wa bariadi
‘’Alisema Meneja kiongozi Jonh Mwalisu .
Meneja
Kiongozi Mwalisu alisema kuwa mikoa mingine itakayo husika katika zoezi hilo ni
Kuanzia october 17 hadi 21 nipamoja na Mikoa ya nyanda za juu kusini ambapo
aliitaja mikoa hiyo nipamoja na Mbeya,Iringa pamoja na Rukwa .
Alisema kuwa
zoezi jingine la uhakiki wastaafu linatarajiwa kufanyika Oktober 24 hadi 28
katika mikoa ya Arusha,kilimanjaro ,Manyara wakati kanda ya kusini inajumuisha
mikoa ya Mtwara mjini ,Newala ,Masasi ,lindi mjini ,Ruvuma Mjini pamoja na
tunduru inatarajiwa kufanyika kuanzia OKutoba 24 nakuishia okutoba 28.
‘’Zoezi hili
linawataka wastaafu wote kuja nanyaraka zifuatazo Kitambulisho cha mstaafu cha
PPF ,Picha moja ndogo ya rangi ya sasa ,kitambulisho chataifa ,kadi yampiga
kura ama hati ya kusafiria au leseni
yaudereva ‘’Aliongeza Mwasu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni