Alhamisi, 25 Agosti 2016

KITUO CHA SHERIA LHRC CHA MTAKA RAIS MAGUFULI KUZINGATIA HAKI ZA BINADAMU .

Tokeo la picha la hellen kijo bisimba
MKURUGENZI WA KITUO CHA LHRC HELLEN BISIMBA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI .

Timothy Marko.

KITUO  Cha  Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC)kimemtaka Rais wajamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jonh Pombe Magufuli kujenga utamaduni wa kutoa kauli zinazofuata misingi ya haki za binadamu na kuheshimu sheria .


Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa kituo hicho Hellen kijo Bisimba amesema kuwa Rais ananguvu kubwa ya utekelezaji wavyombo vyote vya serikali ikiwa kinyume ,inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mtu mmoja au jamii nzima .

 

''Tunamuomba Rais Magufuli kufuta kauli zake zenye utata ikiwemo kauli ya kufuta  shughuli za kisiasa mpaka 2020 kwani kauli hiyo iko kinyume kabisa na ibara za 3(1)na 2(1)yakatiba na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 pamoja na kanuni za sheria ya vyama vya sisasa 2007'' Alisema Mkurugenzi wakituo cha Haki za Binadamu Helleni Kijo Bisimba .

 

Bisimba alisema kuwa ni wajibu waviongozi waliopo serikalini kulinda nakuheshimu haki za binadamu kama zilivyoanishwa kwenye katiba ya jamuhuri ya Muungano wa  Tanzania na sheria za nchi  kama walivyoapa kuzilinda kwenye kiapo cha uongozi .

 

Alisema sambamba na kumtaka Rais Magufuli kujenga kauli zinzofauata misingi ya haki za binadamu pia amewataka jeshi lapolisi navyombo vya dola kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata sheria na taratibu za sheria na kujipambanua na kutowatisha wananchi nakuwajengea hofu ya umwagaji wa damu .

 

''Kazi kuu ya Jeshi la polisi nikulinda usalama wa raia na mali zao nasio kuwaumiza raia hivyo jeshi lapolisi liache maramoja kuzuia mikutano yandani ya vyama vyasiasa kuzuia wanasiasa nikuingilia uhuru walionao kikatiba na kisheria hususani uhuru ulioanishwa katika ibara 17 yakatiba ya jamuhuri ya muungano .'''Aliongeza Bisimba .

 

Bisimba aliongeza kuwa nilazima vyama vyasiasa  nchini kushindana kwa hoja na kuacha kutumia vyombo vya dola katika kushinikiza hoja au matakwayao ,hii itasaidia kukuza nakuimarisha haki za binadamu na demokrasia nchini .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni