picha ya bomba lamafuta |
Timothy
Marko.
SERIKALI ya
Tanzania kwa kushirikiana nanchi ya Kidemokrasia ya watu wa Congo zimeingia
makubaliano ya ujenzi wa bomba la Mafuta katika ziwaTanganyka ,ambapo ujenzi
wabomba hilo unatarajiwa kuanza mwezi October mwaka huu.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mapema hii leo jijini Dar es salaam Waziri wanishati na
Madini professa Sospeter Muhongo amesema kuwa ujenzi wa bomba hilo unaotarajiwa
kuanza mwezi October mwaka huu unatarajia kuanza katika maeneo ya kabale Uganda
nakwenda zaire ukipitia katika ziwa Tanganyika lilopo mpakani mwa nchi hizo
mbili .
‘’Mafuta pamoja
na gesi yatakayogundulika katika ziwa Tanganyika tunampango wakugawana baina
yanchi hizi mbili yani Congo na Tanzania ‘’Alisema Waziri wanishati na Madini
sospeter Muhongo .
Profesa
Muhongo amesema kuwa kwasasa tayari serikali ya Congo na Tanzania zimekubaliana
kampuni ambayo itakayo jihusisha na uchimbaji itaweza kusafirisha mapipa
20,0000 kwasiku .
Kwaupande
wake Waziri wanishati wanchini Congo Profesa Aime Ngoi Mukena amesema kuwa
ujenzi wa bomba hilo utakao unganisha nchi za Rwanda Uganda na Kongo nimuhimu
kwa uchumi wanchi hizo katika kujenga uchumi kupitia sekta hiyo.
Alisema kuwa
hatua iliyofikiwa nanchi hizo kuungana katika ujenzi wa bomba hilo la mafuta
nagesi unafananishwa kama zawadi kutoka kwa mungu hivyo nivyema nchi hizo
kutumia rasmali hiyo ili kujiletea maendeleo ya kiuchumi
.
‘’Ninayofuraha
Kwa Tanzania Uganda Rwanda kuungana katika ujenzi wa bombahili lamafuta ambapo
mkutano wa makubaliano ya awali yatafanyika mwezi October mwaka huu ni hatua
kubwa kwani hatua hii nizawadi kutoka kwamungu ‘’Alisema Profesa Aime Ngoi Mukena .
Waziri mukena
alisemakuwa hatua hiyo itawezesha kongo kunufaika namafuta kutoka katika ziwa
Tanganyika .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni