Ijumaa, 8 Julai 2016

UNFPA :NDOA ZA UTOTONI HUCHANGIA ONGEZEKO LA WATU DUNIANI

Timothy Marko.
Shirika la umoja wa Mataifa linaloshugulikia idadi ya watu (UNFPA)limesema zaidi ya asilimia 7 ya wasichana walipo kati ya umri wa miaka 15-19 hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kama njia yakudhibiti mimba katika umri mdogo .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salam Muwakilishi mkaazi wa shirilika hilo nchini Dr.Natalia Kanem amesema kuwa hali hiyo imechangiwa na naukosefu wa elimu sahihi na uwekezaji wasichana hao katika utoaji wa elimu ya afya ya uzazi na njia mbalimbali za kuhibiti mimba .

''Jambo jema lakufanya kuwawezesha wasichana kwanjia yaelimu ,ulinzi na maelezo inawezekana katika nchi zinazo endelea ,katika nchi ya Tanzania asilimia saba tu yavijana walioko katika ndoa walio kati yaumri wamiaka 15-19 hutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango ''Alisema Dr.Natalia .

Dr.Natalia alisemakuwa kuwa katika jitiahada zakuwalinda wasichana na mimba za utotoni niagenda muhimu katika ajenda yamaendelo nakuweza kupambana natatizo laongezeko la idadi ya watu nchini .
Alisema ongezeko lavijana katika nchi ya Tanzania ni kubwa ikilinganishwa na miaka ya awali ongezeko hili linaweza kuongezeka katika miaka ijayo .

''Mara nyingi mizizi katika ujinga usawa wakijinsia nandoa za kulazimishwa  ukosefu wa elimu naunyasasaji wa wakijinsia nakutumia nguvu nijambo linalochangia sana ndoa za utotoni naidadi ya watu.''Aliongeza NATALIA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni