Jumanne, 5 Julai 2016

JESHI LA POLISI LAWATAADHALISHA WANANCHI JUUN YA UTAPELI WA MAGARI

Timothy Marko

Jeshi la polisi kanda maalum ya kipolisi Dar Es Salaam, limewataadhalisha wananchi hasa wamiliki wa vyombo ya mato kuwa makini pindi wanapokosha au kuazima vyombo vyao kwa watu.

Onyo hilo limetolewa na kamishna wa kanda maalum ya kipolisi SIMON SIRRO kwa vyombo Lvya habari wakati jeshi hilo lilipopata taarifa kwa mkaazi wa jijini Dar Es Salaam AUFURO MOSHI [42] baada ya kutapeliwa gari aina ya Toyota noah, ambalo lilikuwa likiendeshwa na MSIFU KYONDO kwa lengo la kufanya sherehe.

 Alisema ‘baada ya jeshi hilo kupata taarifa za wizi huo lilituma kikosi cha kupambana na wizi wa magari wa kanda hiyo na kufanikiwa kumkamata RASHID NASSORO marchi 15.2016 huko maeneo ya vijana kinondoni akiwa na gari hilo akidai kuwa ameuzia na TUMSIFU KYANDO.

“Katika tukio lingine lililotokea march 03.2016 majira ya saa 11 asubuhi maeneo ya mnazi mmoja wilaya ya ilala, mlalamikaji CLIFF GEORGE pamoja na mtuhumiwa huyo June 02.2016 majira ya saa 02 usiku katika mtaa wa samora alimkabidhi gari lake Toyota harrier lenye namba za usajili T 468 CC kwa mtuumiwa ALI SALEHE kwa makubaliano aliuze kwa shilingi mil.18, kinyume na makubaliano mtuhumiwa alikimbia na gari kusikojulikana” alisema kamishina SIRRO.


Kamishina sirro alisema baada ya kikosi cha kupambana na wizi wa magari cha jeshi hilo kupata taarifa waliweka mtego na kufanikiwa kukamata gari hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni