KAMISHINA WA TRA ALPHAYO KIDATA AKIZUNGUMZA NA WAAANDISHI WA HABARIJIJINI DAR ES SALAAM (HAWAPO PICHANI) |
Timothy
Marko.
MAMLAKA ya
mapato nchini (TRA)imewagawia Makatibu wa kuu wa wizara mashine tano za EFD
kwa ajili ya kukusanya maduhuli ya serikali kwa mashine hizo.
Hatua hiyo imetokana na agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dk.Jonh Pombe Magufuli ya kutaka Wizara zinazotoa huduma ziwe na mashine za EFD
ili kuweza kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa taifa .
Akizungumza leo na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es
Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa ugawaji wa mashine
hizo kwa taasisi za serikali zitasaidia kutunza
kumbukumbu katika kupanga maduhuli.
“Mashine
hizi ni lengo serikali katika kuhakikisha wananchi wanaopata huduma wanapata
risiti kwa kutambua umuhimu wa kodi kwa huduma wanazopata”amesema Kidata.
Aidha
amesema hizo mashine ni mashine za kwanza katika mashine zote kutokana na kuwa
za kisasa katika kutunza kumbukumbu za huduma ambazo wanazitoa.
Kamishina wa
Mapato ya Ndani wa TRA, Ellijah Mwandumbya amesema kuwa watawafundisha wakuu wa
idara hizo jinsi ya kuzitumia.
zinaendana sambamba
na utoaji wa risiti za EFD kwa watumishi wote wa serikali ambao wanafanya
marejesho ya matumizi mbalimbali katika taasisi hizo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni