waziri wa afya maendeleo yajamii jinsia wazee na watoto. |
Timothy Marko.
SERIKALI
imesema kuwa itaendelea kuweka kipaumbele cha afya yamama namtoto ilkuweza
kuondokana navifo vya mama namtoto ilikuweza kufikia malengo ya milenia ya 2025
yakupunguza vifo vya vitokanavyo afya yauzazi .
Akizungumza
mampema jijini Dar es salaam waziri wa afya maendeleo yajamii jinsia wazee
nawatoto Ummy Mwalimu amesema kuwa sambamba nakuweka kipaumbele kwa afya ya
mamanamtoto pia ,Serikali itaendelea kutilia msisitizo juu yautunzaji wa
mazingira ilikuweza kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu .
‘’Kila katika
mwaka baada yamiezi kumi kumekuwa na ongezeko lawagonjwa wakipindupindu wapatao
345 nchi nzima,hali hii imechangiwa na hali yauchafu katika baadhi yamiji yetu ‘’Alisema
WAZIRI Ummy Mwalimu .
Waziri wa
afya maendeleo yajamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa
jitihada za serikali katika kukomesha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu
haziwezi kufanikiwa endapo serikali hatoweza kuwekeza katika uboreshaji wa
mazingira na afya katika maeneo yanayowazunguka wananchi .
Alisema
kuwa serikali inawataka wananchi
kutojisaidia ovyo nakudhibiti taka ngumu nakunawa mikono kabla nabaada ya kula
chakula.
‘’Hali ya
usafi inaimarika katika kipindi cha hivi karibuni baada ya Rais Magufuli
kuhimiza wananchi kujenga tabia ya kufanyausafi,lakini hadi hivisasa
kunachangamoto ya vifaa vya kuzolea taka ‘’Aliongeza Waziri wa afya maendeleo
yajamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni