Timothy
Marko.
WANASIASA
wametakiwa kutobeza juhudi za Rais Dk.Jonh Magufuli za kuwaletea maendeleo badala
yake wamsaidie kufanya kazi yenye kuleta
mafanikio yenye tija nchini.
Hayo
yamebainishwa na mwanazuoni DK.Haruni Kondo wakati akizungumza na waandishi wa
Habari katika uzinduzi wa kitabu cha uongozi wa awamu yatano na hatima ya nchi
yetu kilicho andikwa na mwanazuoni huyo , mapema hii leo jijini Dar es salam,
ambapo amesema kuwa Rais Magufuli amekuwa akijikita katika misingi ya muasisi
wa taifa hili Mwalimu Nyerere.
‘’Watanzania
tunapaswa kuwa makini na kukataa hadaa na propaganda za baadhi ya wanasiasa uchwara
wabinafsi wenye uchu na uroho wa madaraka ‘’Alisema Mwanazuoni DK.Haruni Kondo.
Mwanazuoni
Kondo alisema kuwa wanasiasa ,wasomi watumishi wa umma na wafanyabishara na
viongozi wadini wamekumbwa na ugonjwa wa husuda .
Alisema kuwa
Wanasiasa pamoja na viongozi wadini wanapandikiza chuki kwa wananchi hao nisumu
kwa mstakabali wa nchi yeyote ile .
‘’Watu wa
aina hii wanapandikiza chuki wana maradhi wanaweza kuleta mpasuko nakisha
kuleta vurugu na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi zao ‘’aliongeza
Mwanazuoni KONDO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni