Jumamosi, 2 Julai 2016

TANZANIA NA RWANDA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA VIWANDA .

Timothy Marko.

WAKATI Mahusiano kati ya Nchi ya Rwanda na Tanzania yakiwa katika hali ya kutoelewana hapo awali kutokana nakile kinachoitwa vita yakiuchumi katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete baada ya Nchi hiyo kuwa na mkakati wa kujenga Reli kutoka Nchi hiyo hadi Afrika kusini ,Hatimaye Rais Jonh Pombe Magufuli amekata mzizi wa fitina baada yakurudisha uhusiano wa kiuchumi na nchi hiyo .



Hali hiyo imeweza kuonekana hapo jana jijini Dar es salaam baada ya Rais wa Nchi hiyo Paul Kagame kufungua maonesho ya 23 ya biashara yakimataifa katika viwanja vyasaba saba vilivyopo jijini Dar es salaam ambapo Rais huyo amesema kuwa niaya Rais Magufuli kuja kukaribisha hapa nchini ni kufufua Mazingira ya biashara baina yanchi hizo mbili.



''Kuja Kwetu hapa ni hatua ya kuboresha Mazingira ya kibishara na kuondoa vikwazo vya kufanya biashara ilikuwezesha kupanua milango yakibishara katika nchinyinginezo zilizopo katika ukanda huu wa afrika Mashariki nanchi nyinginezo zilizo nje yaukanda wa afrika mashariki ''Alisema Rais Paul Kagame



Rais Kagame alisema kuwa uhusiano uliorejea kati ya Tanzania na Rwanda utaleta Mtengamano wa kiuchumi baina yanchi hizo hasa katika kuboresha sekta ya viwanda hata hivyo Rais huyo wa Rwanda aliisifu nchi ya Tanzania kwa kuwa na Rasmali nyingi ambazo zitawezakukuchochea mazingira mazuri ya kiuchumi .

Alisema Hali yautengamano naushirikiano wanchi yake nanchi ya Tanzania itachangia kukua kwa uchumi hasaule wa Viwanda .



Aidha, Katika Hatua nyingine Rais Magufuli amesema hali yaushirikishwaji wa kiuchumi baina nanchi nanchi umepungua katika bara afrika ikilinganishwa na nchi za bara la Asia ambapo kiwango cha ushiriki katika uchumi ni kikubwa .



Alisema Hali hiyo ya kutoshirikiana nanchi nyinginezo zimetokana kutouziana Malighafi wakati alizitaja fursa za kiuchumi zilizopo katika nchi hizo endapo zitatumiwa vizuri zitaweza kukuza uchumi nakusisiza kuwa nchi za afrika Mashariki ziaidadi yawatu Takribani Milioni 105 ambapo fursa hiyo ikitumiwa vizuri itawezesha nchi hizo mbili kukuza uchumi wake .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni