Timothy Marko kwahisani yamitandao.
June 28 2016 Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu alifikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa
ajili ya kujibu tuhuma za uchochezi kupitia gazeti la mawio kwenye
habari yenye kichwa kinachosema ‘Zanzibar Machafuko yaja’ dhidi yake na wenzake watatu.
Nje ya mahakama hiyo Lissu alizungumza na waandishi wa habari ambapo
alitoa kauli ambayo imewafanya polisi wamuite kwa ajili ya mahojiano,.
Lissu
alifika kituo kikuu cha polisi Dar es salaam kuitikia wito wa polisi
na amehojiwa na polisi kwa masaa matatu kutokana na kauli hiyo atalala
rumande leo kwa amri ya ZCO baada ya kukosa dhamana na atafikishwa
mahakamani kesho.
Tundulisu anashuka katika gari la polisi katika viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Tundulisu anashitakiwa kwa kosa la kutoa maneno ya kashifa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni