Katibu MKUU TAMISEMI MHANDISI MUSSA IYOMBE |
Timothy
Marko .
ZAIDI yashilingi bilioni 1.6 zinatarajiwa Kutumiwa
naserikali Katika maboresho ya upatikanaji wa taarifa za wananchi kupitia mfumo
wa kiletroniki ili kuiwezesha serikali kuweza kupanga mpango mbalimbali ikiwemo
kuwa patia huduma stahiki wananchi.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais –TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa mfumo huo utawezsha kupata
taarifa katika ngazi yakitongoji na mtaa .
‘’Mfumo huu
unaotumia Data base umeweza kutumika katika nchi za Botswana,Syecelles,Tanzania
,Zanzibar na Mauritus nan chi ambazo zina idadi yazaidi milioni 1 ,Nchi
nyingine zinaendelea juhudi za kuboresha mifumo yake kama Tanzania ‘’alisema Katibu
Mkuu Mhandisi Mussa Iyombe .
Mhandisi
Iyombe alisema kuwa mfumo huo utawezesha kufanya utambuzi wa Raia kwangazi
yakitongoji na mtaa na kutunza kumbukumbu za rejista za wakaazi wote nchini .
Alisema
Mfumo huo umewahi kutumika katika nchi za ulaya Sweden Norway nanchi Nyinginezo
katika ukanda wa bara la ulaya na amerika .
‘’Mfumo huu
sio jambo jipya kwa nchi yetu tulikuwa na mfumo huu ambao tulikuwa tunatumia
dafutari maalumu la ukaazi kinacho fanyika hivi sasa nimaboresho yataarifa kwa
njia ya mfumo wa kiletroniki ‘’Aliongeza Katibu Mkuu Mussa Iyombe .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni