Mpiga chapa wa SERIKALI Kassian Chiboyo |
Timothy Marko.
Ofisi ya
Mpiga Chapa wa Serikali nchini imewataka Wananchi kuheshimu vielezo vya taifa
ikiwemo Bendera ya Taifa ,wimbo wataifa
na Nembo ya Taifa .
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mpiga chapa wa ofisi wa ofisi hiyo
Kassian Chibogoyo amesema kuwa kwamujibu wa sheria ya bunge ya mwaka 1971 na
sheria ya bendera yataifa ya mwaka 1962 na sheria yangao ya taifa Cap .504
,pamoja sheria ya alama za taifa inamkataza mtu yeyeote kutumia bendera yataifa
nangao yataifa kinyume nailivyokusudiwa .
‘’Sheria
hizi zinamkataza mtu yeyote kutumia bendera ,nembo yataifa au chochote kinacho
fanana na bendera ya taifa na ngao ya taifa kama alama yabiashara au shughuli
za kitaluma au kwenye maandiko yanayokusudia Mauzo ‘’Alisema Kassian Chibogoyo
Mpiga Chapa
wa serikali Chibogoyo alisema kuwa mtu yeyote atakaye kaidi anaweza kuhukumiwa
kifungo kisichozidi miaka miwili .
Alisema kuwa
nikosa la kisheria kutoa lugha ya kashifa au kuandika maneno yenye lengo
lakukashifu bendera au nembo ya taifa kwani unaweza kufungwa kifungo kisicho
zidi miaka miwili .
‘’msisitizo
wa kuheshimu vielezo vya taifa upo katika kanuni ya utumishi wa umma wa mwaka
2009kifungu cha q.20 ambacho kinaonya kuwa bendera ya taifa iliyo tobokatoboka
au kupauka au chafu nimarufuku kutumika ‘’Aliongeza chibogoya .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni