Mkurugenzi wa Kituo cha sheria na Haki za binadamu nchini Hellen Kijo |
Timothy
Marko.
KITUO cha
sheria nchini kimesema haki ya kuishi imekuwa ikikiukwa mbele ya vyombo vya
dola baada ya vyombo hivyo kujichukulia sheria mkononi hali inayochangia watu mbalimbali
kufa wakati wakiwa chini ya vyombo vya dola .
Akizungumza
na waandishi wa habari katika uzinduzi wa ripoti ya hali ya Haki za binadamu
nchini Mkurugenzi wa Kituo cha sheria na Haki za binadamu nchini Hellen Kijo amesema
jumla yawatu 394 walikufa kutokana mauaji yavitendo mateso yavikongwe katika
maeneo ya vijijini .
‘’Ongezeko
hili la 394 nikubwa ikilinganishwa vifo vilivyotokea mwaka 2015 ambapo vifo 57
viliweza kuripotiwa katika kipindi cha mwaka jana ‘’alisema MkurugenzI wa kituo
cha Sheria Hellen Kijo.
Kijo alisema
taarifa za jeshi lapolisi zinaonesha kuwa kumekuwa namatukio ya mauaji kwa watu
kujichukulia sheria mkononi yamekuwa yakipungua ,hata hivyo katika kipindi
chamwaka huu watu 135 waliuwawa kutokana kujichukulia sheria mkononi
.
Alisema japo
taarifa hii haioneshi idadi yawatu waliojeuriwa kutokana kutoka namatukio ya
kujichukulia sheria mikononi matukio haya yanaonekana kuwa mengi .
‘’Matukio ya
vifo kwa kipindi hiki cha nusu mwaka nipungufu sana ikilinganishwa nakipindi
hiki kwa mwaka jana ambapo taarifa zinaonesha vifo vya watu 366 viliweza
kuripotiwa ‘’Aliongeza Bi Hellen KIJO .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni