RAIS MSTAAFU wa awamu ya nne DK.JAKAYA KIKWETE |
Timothy
Marko.
Rais Mstaafu
wa awamu ya nne wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Kikwete
anatarajiwa kupewa tunzo ya amani itakayotolewa na Taasisi ya Maridhiano ya
Tanzania katika viwanja vya KarimuJee julai 13 mwaka huu.
Utoaji watunzo
hiyo kwa Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya KIKWETE ,ambao utahudhuriwa nawaziri wa
Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba w Kama Mgeni Rasmi wa
Maadhimisho ya uzinduzi huo wa tunzo za amani unafuatiwa na Jitihada za Rais huyo mstaafu
katika kuleta utengamano wa amani katika nchi za nje yanchi ikiwemo mgogoro wa
Burundi na Rwanda .
Akizungumza
na waandishi wa Habari Mwenyekiti wa Taasisi ya Mardhiano nchini Sadick Godi Godi amesema kuwa sambamba nautoaji
watunzo hiyo ya amani kwa Rais Kikwete ,pia taasisi hiyo inatarajiwa kutoa
tunzo kwa Mama Maria Nyerere kwa mchango wake katika taifa la Tanzania kama
Muasisi wa taifa la Tanzania namdau wa amani .
‘’Ni mtu wa tatu
anayepewa tunzo ya amani katika taasisi yetu anatarajiwa kuwa Mkuu wa jeshi
lapolisi Mstaafu Said MWEMA ,Mkuu wa jeshi la polisi huyu mstaafu amekuwa
mstari wa mbele katika kusimamia amani kwa kuanzisha polisi jamii ‘’Alisema
Sadick Godi Godi.
Godi Godi
alisema kuwa taasisi hiyo imeweza kutambua mchango wa Mwenyekti wa makampuni ya
IPP Reginald Mengi kama mtu muhimu wa katika kuwasaidia makundi maalum ya watu wenye
ulemavu na kuweza kupatia tunzo hiyo ya amani nchini .
Alisema
wengine watakao pewa tunzo hiyo nipamoja Sabodo kwa mchango wake katika
kuisaidia jamii katika uchimbaji wa visima nakutoa huduma hiyo pasipo
kuzingatia misingi yakidini na kiitikadi .
‘’Bi Hellen
Kijo Bismba ni mtu wasita atakaye pewa tunzo hii ya amani ambapo mwenyekiti
huyu wa kituo cha sheria na haki za binadamu anatajwa kuwa kinara wakusimamia
haki za binadamu nchini ‘’aliongeza Godigodi .
Godigodi
Aliongeza kuwa Wengine wataopewa tunzo hiyo nipamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Sadick Mecksadick ,Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba ,Mwanzilishi
naspika wa bunge la uchumi Tanzania Albert Sanga pamoja mbunge BONA kaluwa .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni