Alhamisi, 28 Julai 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AWATAKA MANISPAA YA TEMEKE KUONDOA WATUMISHI WASIOKUWA NASIFA.


Timothy Marko .
WAZIRI MKUU wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka Manispaa ya Temeke kuhakiki watumishi wenyesifa na kuwaondoa watumishi wasio kuwa nasifa ilikuweza kuboresha utendajikazi wa manispaa hiyo katika ukusanyaji wa mapato ya serikali .

Akizungumza katika ziara aliyoifanya katika Manispaa ya Temeke mapema hii leo Waziri Mkuu Majaliwa aliwapa manispaa hiyo siku mbili kuanzia leo hadi julai 30 mwaka huu kuhakikisha watumishi walikuwa nasifa wanaajiriwa katika manispaa hiyo nakuachana watumishi wasikuwa nasifa .

''Watumishi wasiotimiza wajibu wao nilazima wachukuliwe hatua za kisheria nataka manispaa hizi mbili za kigamboni zinapata mafanikio makuwa katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kwani manispaa hizi mbili ndizo zenye vyanzo vingi vya mapato ''Alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri mkuu Majaliwa alisema kuwa lazima kitengo cha uhasibu chamanispaa hiyo lazima kiwe makini nakutokubali fedha zitokanazo nakodi  za makusanyo mbalimbali yakodi katika manispaa hiyo kuweza kupotea  pasipokuwa na maelezo
.
Alisema kuwa lazima madiwani wamanispaa hiyo kuweza kupunguza matumizi yafedha yasiyo yalazima ikuweza fedha hizo kuweza kutumika kwamatumizi stahiki na kuwataka madiwani kujua makusanyo yafedhahizo zimeingia lini nakuwa na nakala yamatumizi yafedhahizo nakupeleka kwa mkuu wa wilaya hiyo
.
''Nataka sekta yaelimu na afya kuweza kupewa kipaumbele zaidi nakuweza  kupewa kiwango kikubwa chafedha katika bajeti yamanispaa ya temeke ''Aliongeza Waziri Mkuu MAJALIWA .

Katika hatua nyingen WAZIRI mkuu Majaliwa  ameweza kupokea hundi ya shilingi milioni 15 kutoka kwa mkuu wa wilaya manyoni na hundi yashilingi milioni 85kutoka ofisi ya waziri mkuu kwaajili ya mchango wa madawati ilikukabiliana tatizo la uhaba wa madawati unalo likabili shule nyingi nchini .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni