Afisa MWANDAMIZI wa SOKO la HISA Dar es Salaam Mary Kinabo |
Timothy Marko.
KIWANGO cha
Mauzo yahisa katika Soko la hisa Dar es Salaam kimeshuka Kutoka shilingi
bilioni 11.6 ikilinganishwa nashilingi bilioni 5.6 katika kipindi cha wiki iliyopita
hali iliyochangiwa kupanda kwa Sekta ya viwanda kwa asilimia 11.47 baada
yahisa TCCL Kupanda kwa asilimia 0.61 .
Akizungumza
na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Afisa Mwandamizi wa Soko hilo Mary Kinabo
amesema wakati kiwango hicho cha mauzo kikiwa kimeshuka kutokana kupanda
kwasekta yaviwanda kwa asilimia 11.47 kufuatia bei ya hisa za hisaTCCL naTBL kupanda kwa asilimia 0.61 Sekta ya huduma za
kibenki na kifedha imeonekana ikipanda kwa 5.83baada yahisa zilizo kwenye
kaunta katika soko hilo kupanda .
‘’Wakati huo
huo Makapuni yanayoongoza kwa kuuza hisa zake nakununuliwa nipamoja na soko
lahisa la Dar es salaam (DSE) kwa asilimia 61,CRDB Asilimia 34 wakati Kampuni
ya Bia nchini (TBL)ikishika nafasi yatatu kwa asilimia 2.6 kwa kuuza
nakununuliwa hisa zake katika soko hili ‘’Alisema Afisa biashara Mwandamizi
Mary Kinabo .
Aidha,katika
hatua nyingine Afisa Biashara Mwandamizi Kinabo alisema kuwa kufuatiashindano
la kukuza uelewa juu ya masoko yamitaji kupitia soko hilo jumla ya vyuo vipatavyo vitano vimeingia katika
fainali ya shindano hilo huku chuo cha cha elimu yabiashara cha jijini Dar es
salaam (CBE )Kikiongoza kikifuatiwa na chuo cha mipango .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni