MOJA YA MITAMBO YAGESI ILIYOPO MTWARA |
Timothy
Marko.
SERIKALI
imesema itapitia kwa upya mifumo ya kuratibu sekta ya mafuta na gesiasilia
nakutoa muongozo wa utekelezaji wa sekta hiyo ilikuweweza kukuza ushiriki wa
watazania kunufaika na rasmali hiyo .
Akizungumza
na waandishi mapema hii leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu
Dk.Hamisi Mwinyimvua amesema kuwa katika kipindi cha Mwezi Mei mwaka jana
serikali ilipitisha sera yaushiriki wa watanzania katika sekta ya mafuta nagesi
wakati huo huo serikali ilipitisha sheria petroli ambayo inatoa fursa kwa
wanachi kushiriki katika kujenga uchumi kupitia sekta hiyo.
‘’Katika
kipindi cha mwezi September mwakajana serikali iliagiza kupitia ofisi ya waziri
Mkuu kuanzisha baraza la taifa lauwezeshaji ,idara ya ushiriki wa watanzania
katika uwekezaji ,aidha kupitia baraza hilo ilitoa majukumu mbalimbali ikiwemo
kutathimini ushiriki wa watanzania katika sekta zote ‘’Alisema Katibu Mkuu DKT.
Hamisi Mwinyimvua .
Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Mwinyimvua alisema kuwa katika zoezi hilo lakuratibu
ushiriki wa watanzania katika uwekezaji katika sekta mbalimbali ,pia serikali
itaipitia mikataba yakimataifa inayohusiana nauwekezaji mkubwa wandani .
Alisema kuwa
kupitia Baraza la uwekezaji litahakikisha kuwa Tanzania inaongeza thamani ya
uchumi wake kupitia sekta mbalimbali ikiwemo sekta yagesi asilia lengo
nikuhakikisha taifa nawatazania kwa ujumla wanaufaika na uwekezaji wa hapa
nchini .
‘’ilikuweza
kufanikisha zoezi hili serikali imeandaa kongamano la siku mbili litakalo
washirikisha wadau mbalimbali wa ndani nanje yanchi ili kuweza kushauriana
nakujadili masuala mbalimbali yauwekezaji ili kuiwezesha serikali kuweka
mipango madhubuti ya ushikirikishwaji wa watanzania kikamilifu ‘’Aliongeza
Katibu Mkuu Mwinyimvua.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni