Kamishina wa kanda maalum Dar es salaam SIMON SIRRO. |
Timothy Marko
JESHI la polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia Gaitoni
Kimulika (18)na Mbelewa Tumeibesi (27)Wakaazi wa Mbezi kwatuhuma za kukuktwa
nasilaha aina ya Gobore iliyokatwa mtutu na risasi moja ya bunduki aina ya shot
gun .
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina
wa Kanda Maalum Simon Sirro amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa najeshi
hilo,baada yakupata taarifa kwa raia wema kuwa huko maeneo yasinza Kangaruu julai13
mwaka huu, kuna watu walifika eneo hilo wakiwa kwenye bajaji wakiwa na begi
likiwa linasidikiwa kuwa na silaha ndipo jeshi lapolisi liliwakamata watuhumiwa
hao .
‘’Baada yakufanya mahojiano nawatuhumiwa hao moja ya watuhumiwa
hao alimtaja mtuhumiwa mwingine kuwa aliondoka eneo hilo nakwenda Maisha Excutive
lodge iliyopo karibu na eneo hilo nakufanikiwa kumkamata mbelwa Tumeibesi
(27)mkazi wa mbezi Makonde ,watuhumiwa wa hao walipo hojiwa walikiri kufanya
kosa lauporaji katika eneo hilo ‘’Alisema Kamishina Simon Sirro.
Kamishina SIRRO alisema kwa jeshi hilo linaendelea kufanya
upelelezi kuhusiana natukio hilo nawatuhumiwa wanatarajiwa kufikisha mahakamani
hivi karibuni .
Alisema Katika hatua nyingine jeshi hilo limefanya operesheni
maalum nakufanikiwa kuwa kamata watuhumiwa wa uhalifu maarufu panya road
wapatao 53 watuhumiwa hao walikamatwa huko maeneo ya Tabata wakiwa nasilaha
ndogo ndogo ikiwemo sime .
‘’Msako mkali unaendelea watuhumiwa wote wanahojiwa namsako mkali
unaendelea ilikuweza kukomesha vikundi magenge ilikukomesha kundi hili
wanaojiita mbwa mwitu ‘’Aliongeza Kamishina Sirro.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni