Timothy
Marko.
SERIKALI
imesema kuwa inaendelea kufuatialia Mapendekezo ya uboreshaji wa mazingira ya
ajira kwa wageni katika kufanyakazi ikiwemo kufuatilia vibali vya wageni ili
kuweza kukuza mahusiano ya nchi rafiki ambapo taasisi zake zinafanyakazi hapa
nchini.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Mapema hii leo jijini Dar es salaam Kamishina wa Kazi
Hilda Kabisa amesema kuwa serikali imelenga kuwakutanisha wadau mbalimbali ambao
wafanyakazi wake ambao si Raia wa Tanzania ambao wanafanya kazi katika
mashirika mbalimbali hapa nchini .
‘’Suala la
vibali vya ajira kwa wageni limekuja kwa wakati muafaka tunatakiwa kutambua
mazingira ya ufanyaji kazi kwa wageni kwa kubainisha ajira zilikuwa nakibali
kwa wageni nazile sisizo nakibali kwa wageni ‘’Alisema Kamishina wa kazi Hilda
Kabisa .
Kamishina
Kabisa alisema kuwa nivyema waajiri wote nchini wawezekupitia vibali vya ukaazi
vya wafanyakazi wao ambao sio raia watanzania nakuweza kuvihakikiki katika
idara ya uhamiaji ,wizara yamambo yandani ilikuweza kupata taratibu za kufanyakazi
hapa nchini.
.
Alisema kuwa
katika kulifanikisha zoezi hilo serikali ipo tayari kushirikiana na waajiri hao
ilikuweka mazingira rafiki ya wafanyakazi ambao sio raia watanzania kuweza
kufanya kazi hapa nchini .
‘’Sisi
kama serikali tutaendelea kusimamia
majukumu yetu ya kuhakiki vibali vya wageni wanao fanya kazi hapa nchini kama
wanavibali vya kufanya kazi hapa nchini ,hivyo nitoe wito kwa makapuni
kuthibitisha vibali vya wafanyakazi wao kabla hawaja waajiri hapa nchini’’Alisema
Kamishina wa kazi KABISA .
Mkurugenzi
wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Aggrey
Mlimoka amesema kuwa Mkutano huo umelenga kutoa mapendekezo ya utungwaji
washeria kwa ajira kwa wageni .
Alisema
kwakuzingatia umuhimu wamkutano huo chama hicho kimeweza kuwakaribisha wadaumbalimbali
wasekta yaajira kwa wageni ikiwemo idara yauhamiaji ambapo watajadili sheria
mbalimbali za vibali ajira kwa wageni .
‘
katikamkutano huu tutapitia taratibu za utungwaji washeria ya ajira kwa wageni
tumewakaribisha wadau mbalimbali ikiwemo kitengo cha idara ya uhamiaji ambacho
kipo chini ya wizara ya mambo yandani ‘’Alisema Aggrey Mlimoka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni