Katibu Mkuu wa Wizara ya afya maendeleoya jamii wazee na watoto Dk Mpoki Ulisibisya akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani . |
Timothy
Marko.
KIWANGO cha
Kaya Maskini kimepungua ambapo zaidi ya asilimia 45 ya kaya zilizopo nchini
zipo chini ya mstari wa umaskini wa mali ,wakati huohuo kaya zilizopo vijijini
ziko chini yamstari kwa asilimia 16 ikilinganishwa na mjini.
Utafiti uliofanywa na taasisi ya Africa
Academy for Public Heath ulionesha kuwa katika kaya zilizopo mjini, kiwango cha
umaskini kimepungua kwa asilimia 28.9 ikijumuisha mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Utafiti huo
ulibanisha kuwa kumekuwa na utofauti katika matumizi ya vyakula mbalimbali kwa
kaya maskini kwa jamii ya wanawake ikilinganishwa na kaya maskini kwa wanaume .
Aidha, kaya
zisizo maskini kwa wanawake ni asilimia 63.8 kwa Tanzania Bara wakati asilimia
80.1 ya kaya hizo zilizopo kwa wanawake waishio Zanzibar wanaishi katika hali
ya umaskini .
Kwa mujibu
wa utafiti huo wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 hutumia virutubishi vya kutosha
vya vyakula vya aina mbalimbali ikiwemo mafuta ,unga wa ngano,unga wa mahindi ,chumvi
na vyakula vinginevyo.
KATIKA hatua
nyingine yajamii jinsia watoto na wazee
Dk.Mpoki Ulisbisya amesema kuwa serikali itaendela kutumia utafiti huo katika
kupanua wigo wa matumizi ya vyakula vyenye virutubisho vya madini na vitamini
iliukuweza kuimarisha afya ya wananchi
.
Dk.Ulisibisya
amesema kuwa serikali ya awamu yatano inatambua umuhimu wa mchango wakuongeza
virutubishi kwa ajili yakuboresha afya nalishe ilikuweza kuinua elimu na uchumi
.
‘’katika
kutambua umuhimu wa utafiti huu serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani
kwenye virutubishi vya vitamin namadini vinavyo agizwa kutoka nje ya nchi kwa
ajili yakuongeza kwenye mafuta yakula ,ungawangano ,unga wamahindi na chumvi na
vyakula vinginevyo ‘’Alisema Katibu Mkuu Dk.Ulisibisya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni