Timothy
Marko.
MAMLAKA ya
Vitambulisho vya Taifa nchini (NIDA )imesema kuwa ifikapo Desemba 31mwaka huu
itatoa Namba yautambulisho itayowezesha kila mwananchi kuweza kutambulika
ilikuweza kurahisisha huduma mbalimbali ikiwemo shughuli za usafiri wandani
nanje ya nchi .
Akizungumza
na waandishi wahabari mapema hii leo Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji Vitambulisho
Alphonce Malibiche amesema kuwa mamlaka hiyo inatarajia kusambaza mawakala wake
wapatao 106 katika maeneo mbalimbali ikiwemo vijijini ili kuweza kurahisisha
zoezi la upatikanaji wa vitambulisho vya
taifa .
‘’Tunatarajia
kusambaza mashine 5600 kwajili yauandikishaji wavitambulisho katika maeneo
mbalimbali vijijini ambapo jumla ya maafisa 106 watahusika katika utekelezaji
wazoezi hili hivi karibuni ambapo mfumo huu wauandikishaji utajumuisha mifumo
ya uandikishaji wa tume yauchaguzi ‘’.Alisema kaimu zalishaji Vitambulisho Alphonce
Malibiche .
Kaimu
Mkurugenzi Uzalishaji Vitambulisho Malibiche alisema kuwa kufuatia kusimamishwa
kwa vijana waliosimamishwa katika mamlaka hiyo mamlaka hiyo inangalia utaratibu
wa kuwalipa stahiki zao ambapo jumatano ijayo wanatalipwa stahiki hizo.
Alisema kuwa
taasisi yake haina ubaguzi katika utoaji wavitambulisho ambapo ucheleweshwaji
wa baadhi ya vitambulisho kwa wananchi unatokana na kuhakiki taarifa
zilizojazwa awali ikiwemo umri pamoja na makazi ya muhusika .
‘’Tunataka
tujiridhishe kabla yakumpa mtu kitambulisho cha uraia hii inatokana
nakuwepo mikanganyiko ya taarifa
zinzotokana utofauti wanyaraka zilizowasilishwa na muhusika ‘’Aliongeza Alphonce Malibiche.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni