Ijumaa, 10 Juni 2016

JESHI LA POLISI DAR LAMSHIKILIA MKAZI DAR KWATUHUMA ZA KUMTUPA MTOTO CHOONI.


Tokeo la picha la kamishina sirro
KAMISHINA  SIMONI SIRRO.
Timothy Marko.
JESHI la  Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam linamshilikilia Rosemary Khiwili (23) Mkazi wa kimara ambayepia nimfanyakazi wa Hoteli ya Landmark jijini hapa kwatuhuma za kumtupa mtoto wake katika choo cha shimo katika nyumba anayoishi .

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo Kamishina wa jeshi la kanda maalum Dar es Salaam Simoni Sirro amesema kuwa mtoto huyo mchanga aligunduliwa akiwa ametupwa katika maji machafu baada ya msamaria mwema Upendo Mboma kuingia katika choo hicho ndipo aliposikikia sauti yamtoto akiwa analia kutokea choo hicho.

''Mtoto huyu aliokolewa na Kikosi cha zimamoto na ukoaji  cha jeshi lapolisi kwa kushirikiana na jeshi lapolisi mtoto huyo amehifadhiwa katika hospital ya  Mwananyamala kwa uangalizi zaidi  upelelezi zaidi unaendelea  naukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi  ''Alisema Kamishina Simon Sirro.

Katika hatua nyingine jeshi hilo juni 8 mwaka huu linawashikilia watu wawili wakaazi wa kunduchi pwani wakiwa namifuko yasukari kumi nasaba ambapo kila mfuko mmoja ulikuwa naujazo wa kilogramu 50.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni