Timothy
Marko.
MAMLAKA ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) imewatoa hofu
wananchi kuwa mvua zinazoendelea ni zakawaida
hazina madhara ambazo huanza mwishoni mwa mwezi Mei na kuishia Agosti mwaka huu .
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa
utabiri, Samweli Mbuya, alisema kuwa hali ya mvua hizo zinatokana na hali ya joto
katika ukanda wa bahari ya pasifiki kupungua na kusababisha baridi kali
inayoambatana na mvua .
‘’Eneo la
kusini mwa Afrika kiwango cha joto Kitaweza kupungua ambapo maeneo mengi
yatakuwa na joto la wastani ambapo katika nchi yetu tunategemea maeneo katika
mikoa ya Mbeya Iringa Pwani na Dar es salaam, ‘’Alisema Mbuya.
Mbuya alisema kuwa katika maeneo nyanda za juu
kusini hayataendelea kuwa nahali yabaridi isipokuwa katika mkoa wa Mbeya .
Alisema
lengo lakutoa tahadhari hiyo nikutoa taarifa kwawatumiaji wa usafiri wa maji
ikiwemo bahari wanajihusisha nashughuli za usafiri na uvuvi pamoja nautalii
ikuweza kupanga mikakati yao kwakuzingatia hali ya hewa nakuweza kujenga uchumi
.
‘’Hali yajoto ina tofautiana na eneo jingine
ambapo tunatarajia kiwango cha joto katika mikoa mingine kinatarajiwa kuwa
sentigradi 29 wakati katika mikoa yapwani inatarajiwa kiwango cha joto kitakuwa
sentigradi 12C’’Aliongeza Mbuya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni