Timothy
Marko.
HATIMAYE
Soko la hisa la Dar es saalam (DSE)imeiorodhesha Benki ya Mucoba katika
makapuni yanayonunua hisa zake kupitia soko hilo ambapo jumla hisa 8,156,423
zimeweza kuuzwa kwa shilingi 250kwa bei yahisa moja .
Akizungumza na
waandishi wahabari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Benki ya
Mucoba Beni Mahenge amesema kuwa upatikanaji wahisa hizo zimetokana juhudi
mbalimbali za wanahisa kuwekeza katika benki hiyo ambapo benki hiyo ilkuweza
kukuza mtaji wake wa shilingi 2,039,105 ,750 .
‘’Kuweza
kuorodheshwa kwa benki hii katika orodha yamakampuni yanayouza hisa zake
kupitia soko lahisa la Dar es salaam DSE hii imetokana kuwepo kwa sera nzuri za
kifedha zinazohamasisha uwazi katika kuwekeza katika kampuni hii ‘’Alisema
Mkurugenzi Beni Mahenge .
Mkurugenzi
Mahenge alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kuorodheshwa katika soko hilo lahisa
la Dar es salaam utawezesha kukuza wigo mpana wa muwekezaji ambaye atanunua
katika masoko mbalimbali yamitaji nakuweza kuuza hisa hizo katika masoko
mengine yakifedha .
Alisema
ilikuweza kununua hisa hizo muwekezaji anaweza kununua hisa zinzouzwa na benki
hiyo kwa kupiga namba *150*36# kutoka kwenye orodha yamakampuni yaliyorodheshwa
katika soko hilo .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni