Kaimu Kamishina wa Idara ya uhamiaji Abbass Irovya akizungumza na waandishi wahabari (hawapo pichani ) Mapema hii leo jijini Dar es salaam. |
Timothy
Marko .
TAKRIBANI ya
Wahamiaji haramu 4,792 wamekamatwa na idara ya uhamiaji nchini ambapo katika kipindi
chamwezi april jumla wahamiaji 1,796 waliweza kufukuzwa kutokana na kutokidhi
Masharti ya kuishi nchini .
Akizungumza
na waandishi wa Habari Mapema hii leo jijini Dar es salaam Kaimu Kamishina wa Idara ya uhamiaji Abbass Irovya amesema kuwa wahamiaji 132 wamefunguliwa mashitaka na kupelekwa mahakamani
kutokidhi Masharti ya kuishi nchini .
‘’Kesi za
wahamiaji haramu takribani 385 zimeweza kufunguliwa nakuendelea kufanyiwa uchunguzi wakina ambapo takribani wahamiaji
haramu 388 wameweza kulipa fani katika kipindi cha Mwezi Novembar mwaka jana
hadi kufikia june mwaka huu ‘’Alisema Kaimu Kamishina Abbas irovya .
Naibu
Kamishina irovya alisema kuwa takribani kesi 509 zinaendelea kufanyiwa upelelezi
ambapo hadi hivisasa Takribani Wahamiaji 294 walikutwa hawana hatia .
Alisema kuwa
sambamba na kufanya operesheni hiyo yakuwa baini wahamiaji haramu idara hiyo ya
uhamiaji inaendelea kufanya oparesheni maalumu yakuwa baini wageni waliopatiwa
vibali vya ajira pamoja nakuangalia vibali vya ukaazi wa wahamiaji hao .
‘’kila
mwajiri kilamwaka anatakiwa kutoa taarifa ya ukaazi kwa wahamiaji walioajiriwa
katika sehemu mbali mbali kabla yarobo tatu yamwaka haija isha ambapo waajili
wasio timiza vigezo hivyo watafikishwa kwenye vyombo vyasheria hii inaendana
nasheria namba 8 yauhamiaji yamwaka 2015 ambapo mtuhuhumiwa akishindwa atalipa
50,0000’’Aliongeza Irovya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni