Alhamisi, 12 Mei 2016

TADB:UKOSEFU WA TAARIFA SAHIHI NI KIKWAZO CHA WAKULIMA KUPEWA MIKOPO KATIKA TAASISI ZA FEDHA.


Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo Thomas Samkyi 
Timothy Marko
Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini imesema kuwa wakulima wengi nchini wanakabiliwa na tatizo lakuto angaliia kilimo kama fursa yakiuchumi  hali inayochangia kutokuwa nauelewa mkubwa katika kujihusisha katika taasisi za kifedha.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji benki ya maendeleo ya kilimo Thomas Samkyi amesema kuwa ukosefu wa taarifa za mauzo za mazao kwa baadhi yakulima ilikuweza kupatiwa mikopo imekuwa nikikwazo kikubwa kinacho wakwamisha wakulima wengi .

"Wakulima wengi hawana taarifa sahihi za mapato zinazotokana na mazao hali inayosababisha taasisi nyingi za kifedha kushindwa kuwapatia mikopo kwa wakulima, "Alisema Mkurugenzi Thomas Samkyi .

Mkurugenzi Samkyi alisema kuwa kutojihusisha katika vikundi vya kupatiwa mikopo imekuwa nikikwazo kikubwa kwa wakulima hao kuweza kupatiwa mikopo yenye mashariti nafuu .

Alisema kuwa wakulima wengi wamekuwa wakitoa dhamana yanyumba ambazo hazina ubora ili kuweza kupatiwa mikopo hali inayochangia wakulima wengi kunyimwa mikopo katika taasisi za fedha .

"Wakulima wengi wamekuwa nanyumba ambazo hazina ubora hazina hati hali inayochangia wakulima wengi kutoweza kupatiwa mikopo "Aliongeza SAMKYI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni