MAUZO YAHISA DSE YASHUKA
Timothy Marko.
MAUZO katika Soko la Hisa (DSE) yameshuka kwa asilimia 59 kutoka sh.bilioni 6.84 hadi kufikia
shilingi BIion 2.8 ambapo Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimeshuka kwa asilimia 26 kutoka milioni 3.8 hadi kufikia Milioni 2.8.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam mapemahii leo, Meneja Mauzo na Biashara Patrick MususaAmesema kushuka kwa mauzo katika soko hilo kumechangiwa na kupungua ukubwa wa Sekta ya huduma za kibeki na kifedha kwa pointi 7.87.
Mususa amesema kampuni zilizoongoza kwa mauzo katika soko hilo ni pamoja na Benki ya CRDB kwa Asilimia 92.40, ikifwatiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 4.16 na Benki ya maendeleoya wakulima (MBP) kwa asilimia 1.61.
Amesema ukubwa wa mtaji wa Soko umebaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 22 ambapo wa mtaji wa makampuni ya ndani umeongezeka kwa asilimia 1 hadi kutoka Trilioni 8.4 hadi kufikia Trilioni 8.4.
Aidha alisema Viashiria katika Sekta ya viwanda vimeongezeka kwa pointi 36.26 baada ya bei za hisa za TOL na TBL kupanda kwa asilimia 3.75 na 1.14 ambapo sekta ya huduma za kibiashara zimebaki kwenye kiwango kile kile cha sh. 3,697.92.
Wakati huo huo msusa alisema jumla ya wanafunzi Vyuo Vikuu waliojiunga katika shindano la (Scholar Investment Challenge 2016) linalo endeshwa na taasisi hiyo wamefikia 3,160 kutoka katika vyuo mbalimbali nchini.
Alisema kuwa mwanafunzi aliyekuwa anaongoza katika shindano hilo wiki iliyopita alifikia mtaji wa sh.1,117,585, ambapo mtaji wake umeshuka hadi kufikia sh. 1,112,135.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni