Jumanne, 15 Machi 2016

TRIONI 2.17 ZA UJAZO WAGESI ZAGUNDULIWA KATIKA BONDE LA MTO RUVU.





Tokeo la picha la sospeter muhongo
WAZIRI WANISHATI NA MADINI  Profesa SOSPETER MUHONGO.

Timothy Marko.
SERIKALI kupitia wizara yanishati namadini imesema kuwa jumla trioni 2.17za ujazowa gesi  zimegunduliwa katika eneo la  Mamba kofi Bonde la Ruvu mkoani pwani .
Akizungumza mapema hii leo jijini Dar es salaam  Waziri wanishati na madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa hadi kufikiamarch mwaka huu jumla gesi yote iliyogunduliwa nitrioni 10.71

‘’Katika eneo la baharini kunagesi nyingi sana hadi hivi sasa jumla ya Trioni 47.78imeweza kupatikana wakati huo huo zaidi ya trioni za ujazo 57.2 zimeweza kugunduliwa kama gesi asilia  ‘’Alisema waziri  Sospeter Mhongo.

Waziri Sospeter Mhongo Alisema kuwa takribani futi zaujazo trioni moja zina uwezo wakuzalisha jumla ya megawati za umeme zipatazo 5000 wakati huo huo ameongeza kuwa bado wanaendelea nautafiti wa gesi katika maeneo yakusini mwa Tanzania kwani kumegundulika kuwa na gesi nyingi .

Alisema kuwa kabla ya awamu ya tano ya Rais Jonh Pombe Magufuli jumla megawati 700 ndizo zilikuwa zikitumika katika kuzalisha umeme lakini katika kipindi cha Rais wawamu yatano jumla megawati 1000 zimeweza kupatikana .

‘’jumla yaviwanda vipatavyo 37 ikiwepo kiwanda chawazo hili kimekuwa kikitumia gesi katika kufanya shughuli zake za
uzalishaji wa umeme ‘’Aliongeza Waziri Mhongo .

kwa upande wake meneja utafiti wa shirika la maendeleo ya mafuta nagesi (TPDC) Venosa Ngowi amesema kuwa jumla yaviwanda 37 vinatumia gesi hadi hivi sasa ikiwemo  kiwanda cha wazo hill .

Venosa alisema kuwa wanatarajia kumpatia ripoti ya mapendekezo ya juu ya gharama za uzawaji wagesi nchini ifikapo mwezi april20 mwaka huu.

‘’zoezi linalofanyika nimazungumzo ya wawekezaji na watalamu wanchi husika kuweza kufanya uhakiki wa gharama wa bei za gesi nchini ‘’AlisemaMENEJA utafiti TPDC  Venosa ngowi.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni