Jumatatu, 1 Februari 2016

JAJI OTHUMANI CHANDE ATOA SIKU SABA KWAMAHAKIMU WASIO KIDHI VIWANGO

https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/f/f9/Mohamed_Chande_Othman.jpg

JAJI WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA .



Timothy Marko.
JAJI Mkuu wa mahakama kuu ya Tanzania Jaji Othman Chande ametoa siku saba kwa majaji  wafawidhi kuchambua na kuanisha mahakimu wote walioshindwa kufikia kiwango cha kesi walizopaswa kuamua nakufikia kesi 250 hadi kesi 260 kwa mwaka 2015,pamoja na kuwataka watoe maelezo ndani ya siku saba kwanini wasifunguliwe mashtaka ya nidhamu na kuwajibishwa.

Jaji Chande alisema kuwa kiwango cha kesi kwa kila hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi na mahakama ya wilaya ni 250,na mahakimu wakazi 121 kwenye mahakama za hakimu mkazi na  Mahakama za wilaya,wameamua kesi chini ya 100 kwa mwaka 2015.
Aliongeza kuwa kiwango cha kesi kwa kila Hakimu wa Mahakama ya mwanzo ni 260,ambapo mahakimu wakazi na mahakimu wa mahakama za mwanzo ni ni 387 wameamua kesi chini ya 100 kwa mwaka 2015.
Alifafunua kuwa uchambuzi,uchunguzi wa mashtaka ya nidhamu ukiondoa wale ambao wameajiriwa karibuni,wanaofanya kazi kwenye mahkama za mwanzo zisizokua na mashauri mengi,au waliokwenda masomoni katikati ya mwak,au likizo za ujauzito.
Aidha alisema mashtaka ya nidhamu kifungu cha 50 na 51 cha sheria ya uendeshaji wa mahakama (judiciary administration act,namba 4 ya mwaka 2011 zimeanzisha kamati za maadili za mahakimu za mikoa na wilaya.

Alitaja kamati hizo ni kamati ndogo za tume ya utumishi wa mahakma iliyoundwa chini ya ibara 112 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,mwaka 1977 kam mojawapo ya majukumu yake kusimamia nidhamu na utendaji kazi mzuri wa mahakimu ibara 113 (1) E.
“mahakimu wote walioshindwa kufikia malengo ya mwaka la kesi na kushindwa kutoa sababu za kuridhisha kwanini wameamua idadi ndogo ya kesi kuliko walivyopaswa watafunguliwa mashtaka ya nidhamu na mashtaka yatashughulikiwa haraka na kamati za maadili za mahakimu kwa mujibu wa sheria na taratibu za haki’alisema 
Alibainisha kuwa uwajibikaji ni hatua muhimu katika mazingira ya sasa ambapo kuchapa kazi na uwajibikaji ni kauli mbiu ya utumishi wa umma’ambapo katika mazingira hayo mahakama ilianza maboresho na kufanya kazi kwa mikakati na malengo tangu mwaka 2013,mahakimu wasiofikia malengo wamekua kama nanga inayozuia jahazi letu kufikia kule tunakotoka kulipeleka kwenye sifuri.
Hatahivyo alisema kuwa mahakama haitavumilia hakimu yeyote anayebembeleza kesi,hivyo hakimu haitakiwi kubembeleza kesi bali inatakiwa amalize kesi kwa wakati





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni