Jumapili, 31 Januari 2016

DSE YAWATAKA WANAFUNZI WAVYUO VIKUU NCHINI KUSHIRIKI KATIKA SHINDANO ILIKUPATA FURSA YA AJIRA



Timothy Marko.
SOKO la hisa la Dar es salaam(DSE) limewataka wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuweza kushiriki katika shindano la scholar Investment Challenge ilikuweza kujipatia fursa ya kuajiriwa katika taasisi za kifedha .

Akizungumza Meneja Mauzo na Biashara wa soko hilo Partick Mmsusa amesema katika shindano hilo linalotarajiwa kuanza mwezi April hadi juni mwaka huu litawezesha wanafunzi wa vyuo wanaoshiriki shindano hilo kuweza kupewa mtaji unaotokana nauwekezaji wa hisa kwa kununuahisa za makapuni mbalimbali zinazo uza hisa zake kupitia soko hilo .

‘’Shindano hili la Scholar Investment Challenge litawezesha  wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kuweza kupata fursa ya kuajiriwa katika Taasisi za kifedha ikiwemo CRDB pamoja FDC ‘’Alisema Patrick Mmsusa .

Meneja Biashara Mmsusa alisema kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ajira pindi wamalizapo masomo yao chuoni hivyo kwakutumia fursa hiyo wataweza kuajiriwa nataasisi za kifedha nakujiajili wenyewe .

Alisema Mwanafunzi wachuo anaweza kujiunga nashindano hilo kwakutembelea tovuti ya soko hilo ambayo ni info.dse.co.tz 

‘’shindano hili nila kila mwanafunzi aliye katika vyuo vikuu vinavyotambulika naserikali ,baada yashindano hili mwanafunzi atapata fursa mbalimbali zakujiliwa na taasisi zakifedha’’Aliongeza Mmsusa .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni